NINI ITIKADI YA MASHIA JUU YA UISLAMU?

NINI ITIKADI YA MASHIA JUU YA UISLAMU?

Mashia kama waislamu wengine, wanaamini kwamba Uislamu ni dini iliyofundishwa na manabii na mitume wote, ambayo mafundisho yake yalikamilishwa na Mtume wa Uislamu - Muhammad (s.a.w.). Uislamu ndio dini pekee sahihi inayokubaliwa mbele za Muumba. Dini zingine zinatokana na uchakachuzi uliofanywa na baadhi ya watu kwa manufaa yao ya kidunia.


Dini hii itaendelea kuwepo mpaka siku ya Kiyama, “Na mwenye kufuata dini isiyokuwa ya Islamu, basi haitokubaliwa  kwake, na (siku ya) Akhera atakuwa miongoni mwa waliopata hasara.” (Qur’ani, 3:84).

Comments