NINI ITIKADI YA MASHIA
JUU YA UKAFIRI NA UISLAMU?
Mashia wanaamini kwamba
Mwislamu ni mtu yule ambaye anashuhudia shahada mbili, “Hakuna Mungu ila Mwenyezi Mungu Mmoja, na Muhammad ni Mtume Wake.” Isitoshe, anafuata maamrisho yaliyoletwa na Mtume
Mtukufu (s.a.w.) kutoka kwa Mola Wake.
Mtu huyu anastahiki
kupewa hifadhi ya nafsi yake, mali na heshima yake na huwa ametakasika. Mambo
yanayowahusu Waislamu yanamhusu yeye pia, vile vile mambo yake yanawahusu
Waislamu wote.
Kafiri ni yule anayekataa
shahada yoyote kati ya hizi mbili, au anakataa jambo lolote katika mambo ya Kiislamu ambalo linajulikana
kuwa ni miongoni mwa mafundisho ya Mtume (s.a.w.).
Comments
Post a Comment