QUR’ANI TUKUFU INAKATAA DHANA YA MAWAHHABI NA MASALAFI YA KUONEKANA KWA ALLAH.
Aya ya Qur’ani Tukufu inakataa waziwazi dhana ya kuonekana kwa Mwenyezi Mungu. Allah (s.w.t.) Anasema:
“Macho hayamfikii, bali yeye anayafikia macho…” (6:103)
Tena, wakati Nabii Musa alipolazimishwa na wana Israel kwenda sehemu yake ya Sala na amuombe Allah “Ajidhihirishe kwake,” Qur’ani Tukufu inaandika tukio hili kama ifuatavyo:
“…(Musa) akasema: “Mola wangu nionyeshe (nafsi Yako) ili nikuone,” Akasema: “Huwezi (Ukathubutu) kuniona…” (7:143).
TAFAKARI HAYA:
1. Kama Qur’an inasema Allah hafanani na chochote kwa nini Mawahhabi wanaamini kuwa Allah ana miguu na mikono?
2. Kinachoonekana kina mwili na kila chenye mwili ni kiumbe sasa mbona mawahhabi wanadai Allah ataonekana?
3. Je huu sio ukafiri wa wazi?
Comments
Post a Comment