SAUMU YA SIKU YA ASHURA

SAUMU YA SIKU YA ASHURA
Katika Sahih Bukhari ipo hadithi inayotokana na mama yetu, bi Aisha kwamba kasema kabla ya kuja dini ya Islam, Maqureishi siku ya Ashura (mwezi 10 Muharram, mfungo nne) walikuwa wakifunga (kutokula) siku hiyo, na Mtume (s.a.w.w.), alipokuja Madina vile vile akifunga na akiwaambia wengine vile vile wafunge, lakini ilipofika mwezi wa Ramadhani na kwa amri ya Mwenyezi Mungu mwezi ukawa faradhi (lazima) Waislamu kufunga basi kufunga siku ya Ashura akawacha (asifunge).
Imepokewa kwamba Abdullah bin Mas’ud (siku ya Ashura) alikuwa akila mara Ash’as akatokea kumwona Ibn Mas’ud anakula akasema, “Kabla mwezi wa Ramadhani haukuwa fardhi kufunga hapo siku ya Ashura ikifungwa lakini tangu kuwa lazima kufunga Ramadhani basi Ashura ikawachwa. Njoo ule pamoja nami.”
MASWALI:
1. Je kuna usahihi katika hadith hii?
2. Je wale wanaofunga swaumu ya Ashura na kusherehekea katika zama hizi wanamfuata nani?
3. Kwa kuwa siku hii ni siku kilipoangamizwa kizazi cha Mtume katika Karbala, huoni kuwa hao wanaofunga na kusherehekea siku hii hufurahia mauaji haya na kwamba wao ndio waliohusika na kukafyeka kizazi cha Mtume?
4. Je Mtume anawapenda watu hao, hata kama wakidai kuwa nao ni waislamu kama sisi Mashia ambao huomboleza sana katika siku hii?

Comments