SWALA BILA KUWASWALIA AHLULBAYT
HAIKUBALIWI NA ALLAH
Dailami anaandikwa kwamba, Mtume
alisema: “Sala zetu hubakia zimezuiliwa mpaka tuombe Swalawat juu ya Mtume na
Ahlul (watu) wake”.
Imam Shafi’i anasema: Enyi Ahlul Bait (watu wa
Nyumba ya Mtume) Allah Amefanya mapenzi kwenu kuwa ni wajib (lazima) kwetu sisi
katika Qur’ani Tukufu. Kwa mintarafu ya ubora wenu, Cheo na Sifa zenu, inatosha
kujua kwamba kama mtu hakuomba Swalawat (rehema) kwa ajili yenu, Sala yake
haikubaliwi.”
Kama Swalawat kwa ajili ya Mtume
na Dhuria (kizazi) wake inaachwa kwa makusudi, basi swala hiyo ya wajib
inakataliwa. Na Mtukufu Mtume amesema: “Sala ya wajib ni nguzo ya imani; kama
Sala ikikubaliwa, matendo mengine yote (ya ibada) yanakubaliwa; kama
imekataliwa, matendo yote mengine yanakataliwa.”
Kuomba Swalawat kwa ajili ya
Ahlul-Bait ni Sunna iliyokokotezwa na ni namna ya ibada ambayo ilikuwa
ikifanywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.
Sisi Mashia tunaona fahari
kufanya kile ambacho Qur’ani Tukufu na Mtume (s.a.w.w.) wametuarimsha sisi
kufanya.
Swalawatu
Comments
Post a Comment