UDHAIFU WA IMANI YA KIWAHHABI NA KISALAFI

UDHAIFU WA IMANI YA KIWAHHABI NA KISALAFI
Bukhari, katika Sura ya “Kitab-e-Ghusl,” na Muslim katika Sehemu ya 2 ya Sahih yake (Sura ya fadhil za Mtume Musa), na Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Sehemu ya 2 uk. 315, na maulamaa kiwahhabi na kisalafi wengine wamemnukuu Abu Huraira akisema:
“Miongoni mwa wana wa Israel ilikuwa ni desturi yao kuoga pamoja bila nguo, hivyo kwamba kila mmoja aliangalia utupu wa mwenziwe. Hawakufikiria kama kuna kizuizi katika hilo. Mtume Musa ndiye aliyekuwa akiingia kwenye maji peke yake, hivyo kwamba hakuna aliyeweza kuona sehemu zake za siri.
“Wana wa Israeli walizoea kusema kwamba Mtume Musa alikuwa na hitilafu katika sehemu zake za siri, na ndio sababu ya yeye kujiepusha kuoga nao.
Siku moja Mtume Musa alikwenda mtoni kuoga. Alivua nguo zake, akaziweka juu ya jiwe na akaingia mtoni. Lile jiwe likakimbia na nguo zake. Musa akalikimbiza lile jiwe akiwa uchi, akipiga makelele: ‘Nguo zangu! Ewe jiwe nguo zangu.’ Wana wa Israel wakamuona Musa akiwa uchi na wakasema: ‘Kwa jina la Allah, Musa hana hitilafu katika tupu zake.’
Kisha lile jiwe likasimama, na Musa akarudishiwa nguo zake. Kisha Musa akalipiga lile jiwe kwa nguvu sana kiasi kwamba lile jiwe likalia kwa sauti kubwa mara sita au mara saba kwa maumivu.”
Kweli mnaamini kitu kama hicho kinawezekana kwa Nabii Musa (A.S.), au kwamba jiwe, kitu kisicho na uhai, lingeweza kuchukua nguo zake? Kwa hakika itakuwa haiwezekani kwa Mtume kukimbia uchi mbele za watu.
Tafakari haya:
1. Je hamuoni kuwa kwa imani yenu hii mmemdhalilisha Mtume wa Mwenyezi Mungu?
2. Je huo sio ukafiri?

Comments