UKAFIRI WA MAWAHHABI NA MASALAFI

UKAFIRI WA MAWAHHABI NA MASALAFI
Wao wanadai yafuatayo kuwa ni miongoni mwa sifa za Allah (s.w): Allah huchukua mwili wa kibinadamu (au kuingia katika mwili wa mwanadamu), kama kiumbe mwenye mwili, anaweza kuonekana katika ulimwengu huu, au ataonekana katika ulimwengu ujao wa Akhera.
Soma kwenye vitabu vya Masalafi na mawahhabi, hususan Sahih Bukhari, Juz. 1, uk. 100 katika Mlango wa Fadhla-s-Sujud Min Kitabu’l-Adhan, na katika Sahih Muslim Juz. 4, uk. 92 Babu’s-Sira Min Kitabu‘r-Riqaq na vilevile tena kwenye hiyo Sahih Muslim Juz. 1 uk. 86 Sura ya Isbatu’l-Ruyatu’l-Mu’Minin Rabbahum Fi’l-Akhira; na Musnad ya Imam Hanbal Juz. 2, uk. 275.
Kwa mfano, Abu Huraira anasema: “Makelele na kishindo cha ukali wa moto vitakithiri, hautatulia mpaka Allah aweke mguu Wake humo. Kisha Jahannam itasema: “Basi, basi! hiyo inanitosha; inanitosha.”
Vilevile Abu Huraira anasimulia kwamba kikundi cha watu walimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); “Je, tutamuona Muumba wetu hiyo Siku ya Malipo?” Akajibu: “Bila shaka. Je, wakati wa mchana wakati anga inapokuwa halina mawingu, jua lina kuumizeni wakati mnapoliangalia?” Wakasema, “Hapana!” Yeye akasema tena: “Je, wakati wa usiku mnapoungalia mwezi mpevu wakati anga ni nyeupe, unakuumizeni?” Wakasema, “Hapana!”
Aliendelea: “Hivyo wakati mtakapomuona Allah Siku ya malipo hamtadhurika, kama vile tu ambavyo hamdhuriki muangaliapo hivi (jua na mwezi). Wakati Siku ya Hukumu itakapofika, itatamkwa na Allah kwamba kila umma wamfuate Mungu wao. Hivyo kila mtu ambaye alikuwa akiabudu masanamu au kitu kingine kisichokuwa Allah, Aliye Mmoja, ataingizwa katika moto wa Jahannamu. Kadhalika kila mmoja wa watu wema na wabaya watalipwa katika moto isipokuwa wale waliomuabudu Allah, Mmoja Mkamilifu. Watalala katika moto wa Jahannamu.
Katika muda huo Allah atatokeza katika umbo Makhususi mbele za watu ili kwamba wapate kumuona. Kisha Allah atawaambia kwamba Yeye ndiye Mola wao. Kisha Waumini watasema, “Tunajikinga na uungu wako. Sisi ni miongoni mwa wale ambao walikuwa hawaabudu kitu chochote isipokua Allah Mwenye mamlaka ya juu.” Allah atasema katika kuwajibu, “Mnayo dalili yoyote kati yenu na Allah ambapo kwamba mnaweza kumuona Yeye na kumtambua?” Watasema, “ndio!” Kisha Allah atawaonyesha mguu wake uliowazi (bila kiatu). Hapo waumini watanyanyua vichwa vyao kuelekea juu na watamuona katika hali ileile kama waliyomuona nayo kwa mara ya kwanza. Kisha Allah atasema kwamba, Yeye ndiye Muumba wao. Wote kwa pamoja watakubali kwamba Yeye ndiye Mola wao.”
TAFAKARI
1. Semeni kweli watu wenye kuiamini sahihi Bukhari na Muslimu ni watu wa madhehebu gani?
2. Je Mawahhabi na masalafi hawaviamini vitabu hivi kuwa ni sahihi zaidi baada tu ya Qur’an?
3. Kama vitabu hivi wanavyoviamini kuwa ni sahihi vimejaa upuuzi wa namna hii, tukisema kuwa hii ndio imani yao tutakuwa tumekosea?
4. Na je watu wenye imani hizi ni waislamu au makafiri?
5. Kama Qur’an inasema Allah hafanani na chochote kwa nini Mawahhabi wanaamini kuwa Allah ana miguu na mikono?

Comments