ULEVI NI HARAMU
Mwenyezi Mungu amesema: "Enyi mlio amini, bila shaka ulevi na kamari na masanamu {ya kuabudu} na mishale {ya ramli} ni uchafa wa kazi ya Shetani. Basi jiepusheni nayo, ili mpate kufaulu. {Qur’an Sura ya 5. aya ya 91}.
Mtukufu Mtume {s.a.w.w} amesema: "Naapa kwa yule aliye niteua na kunipa Utume, kwamba mlevi atakufa hali ana kiu, na kaburini anakiu, na atafufuliwa hali yeye anakiu na atakuwa anapiga kelele 'kiu kiu' kwa miaka elfu; ataletewa {kwa kiu kubwa iliomshika} maji ya shaba iliyoyayushwa itayounguza nyuso zao. Kinywaji kibaya kilioje hicho. Basi utaiva uso wake na kutoka meno yake na kuchopoka macho yake mle katika lile kaburi, na atakuwa hana budi kunywa na huyeyuka yaliyo tumboni mwake."
Comments
Post a Comment