UPOTOFU HUU UTAWAANGAMIZA MAWAHHABI NA MASALAFI

UPOTOFU HUU UTAWAANGAMIZA MAWAHHABI NA MASALAFI
Bukhari anamnukuu Abu Huraira katika Sahih yake (Juz. 1, uk. 158 na Juz. 2, uk. 153), na tena katika Sura ya “Kifo cha Mtume Musa,” na Muslim vilevile anamnukuu huyo huyo (Abu Huraira) katika Sahih yake Juz. 2, uk. 309 katika Sura ya Fadhila za Musa akisema: “Malaika wa Mauti alikuja kwa Mtume Musa na akamtaka akubali mwito wa Mola wake. Aliposikia hivi, Musa alimchapa kofi kali la uso kiasi kwamba jicho lake moja liling’oka.
Hivyo alirudi kwa Allah na akalalamika kwamba amemtuma kwa mtu ambaye hataki kufa, na ambaye amemng’oa jicho lake moja. Allah akaponya jicho lake na akamuamuru arudi tena kwa Musa na amuambie kwamba, kama anataka maisha marefu, yapasa aweke mkono wake juu ya mgongo wa fahali wa ng’ombe. Ataishi miaka mingi kama idadi ya nywele zitakazofunikwa na mkono wake.”
Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Juz. 2 uk. 315, na Muhammad bin Jarir Tabari, katika kitabu chake chaTarikh, Juz. 1, chini ya kichwa cha habari, “Kifo cha Mtume Musa,” ametoa maelezo haya haya kutoka kwa Abu Hurira pamoja na nyongeza kwamba kufikia wakati wa Musa, Malaika wa mauti alikuwa akitoa roho (za watu) katika mwili kiwaziwazi. Lakini baada ya Musa kumchapa kofi la uso, alikuja bila kuonekana.”
Tafakari haya:
1. Sasa ni juu yenu kuamua hiki ni kichekesho au imani?
2. Hivi malaika wa Mwenyezi Mungu ni dhaifu kiasi hiki cha kuchapwa vibao na kushindwa kufanya majukumu yao?
3. Ama kwa Abu Huraira, sizishangai simulizi zake. Maulamaa wa kisunni wanakiri kwamba, ili apate kujaza tumbo lake kwa vyakula vyenye ladha vilivyotolewa na Mu’awiya, alibuni hadithi za uongo. Kwa sababu ya uzushi wake, Khalifa Umar alimpiga viboko. Ni jambo la kushangaza kwamba watu wenye akili wanaamini ngano kama hizi za kuchekesha.

Comments