USHIRIKINA KUHUSIANA NA KISABABISHO
Aina moja ya ushirikina ni ile ambayo huhusishwa kwenye kisababisho, kwa kuwa watu wengi huweka matumaini yao na hofu juu ya kisababisho cha pili. Huu pia ni ushirikina, lakini unasameheka. Ushirikina una maana yakufikiri kwamba uwezo wote kiasili unatokana na kisababisho cha pili. Kwa mfano, jua hustawisha vitu vingi ulimwenguni, lakini kama mtu atafikiria uwezo huu ni wa msingi katika jua (yaani asili yake inatokana na jua lenyewe), basi huu ni ushirikina.
Lakini, kama tunaamini kwamba jua limepata uwezo huu kutoka kwa Allah, na kwamba jua ni kisababisho cha pili tu cha ukarimu wake, basi huu kamwe sio ushirikina. Bali hasa ni namna ya Ibada, kwa kuwa kutafakari juu ya ishara za Allah ni mwanzo wa kumwabudu Allah. Utajo umefanywa katika Aya za Qur’ani Tukufu kwenye ukweli huu kwamba yatupasa kutafakari juu ya ishara za Allah kwa kuwa hii huongozea kwenye mazingatio juu ya Allah.
Kwa njia hiyo hiyo, kutegemea juu ya kisababisho cha pili (nadhari ya mfanya biashara kwenye biashara, au nadhari ya mkulima kwenye shamba lake) humfanya mtu kuwa mshirikina kama kwa sababu hii atageuza mazingatio yake kunyume kutoka kwa Allah.
Comments
Post a Comment