USHIRIKINA ULIOFICHIKA: KUJIONYESHA KATIKA SWALA.
ushirikina uliofichika, ni kama vile kujionyesha katika Swala zetu au namna zingine za utiii kwa Allah. Tofauti kati ya ushirikina huu na ule ushirikina wa katika Swala, ni kwamba kuhusu suala la ushirikina katika Sala tunashirikisha kitu kingine au kiumbe pamoja na Allah.
Kama mtu ataelekeza nia yake kwenye kitu kingine mbali na Allah, katika Ibada ya Sala, au kama kwa ushauri wa Shetani, akawa na picha bandia ya Mungu katika mawazo yake, au kama kiongozi wake ndio kiini cha nia yake, basi ni mshirikina.
Hakuna isipokuwa Allah Ndiye apasaye kuwa mlengwa wa nia katika ibada zetu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba, kama mtu atafanya kitendo kizuri na akafanya mtu mwingine kuwa mshirika pamoja na Allah ndani yake, basi kitendo chake chote ni kwa ajili ya yule mshirika. Allah anachukia kitendo hicho na mtendaji wake pia. Vile vile imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba,
“Kama mtu akifanya ibada ya Sala, au kufunga, au kutekeleza Hija na ana mawazo kwamba kufanya kwake hivyo watu watamsifu, “basi hakika, amefanya mshirika pamoja na Allah katika kitendo chake.”
Comments
Post a Comment