ABUBAKAR NA UMAR WALAZIMISHA MASAHABA KUUKUBALI UKHALIFA WAO WA BANDIA
Abubakr baada ya kutawalishwa alimpeleka Umar bnil Khattab nyumbani kwa Mwana Fatima (a.s.) ili akawatoe wote waende kumbai Abubakr akamwagiza kuwa: Endapo watakataa kwenda kumbai, awauwe.
Umar akaenda na kijinga cha moto, Mwana Fatima alipomuona mlangoni na kijinga hicho akamuuliza: Ewe Umar! Umekuja iwasha nyumba yetu? Umar akajibu Ndiyo Wallahi nitakuunguzeni au mtoke kwenda kumbai Abubakr".
Inasemekana kuwa: Umar alipoingia nyumbani kwa Mwana Fatima, alimpiga ngumi ya tumboni, ngumi ambayo iliumiza ujauzito na kuzaliwa mtoto aliyekufa! Na kwa sababu ya kipigo hicho, afya ya Mwana Fatima ilidhoofu sana na baadaye kufariki. Umar alikuwa akiyakumbuka haya, mwenyewe husema "Laiti ningelikuwa kondoo niliyefugwa, nikanenepeshwa kiasi cha kupendeza. Akija mgeni nikatwekatwe sehemu nyama yangu ikaangwe na sehemu ibanikwe, kisha wanile na wanitoe nikiwa mavi nisiwe binadamu".
Tazama:
Kanzul Ummal J.12 Uk. 619
Tafakari haya:
1. Je Ukhalifa unapatikanana kwa kugombania na kuzozana kama walivyofanya akina Umar?
2. Ukisema ni uchaguzi, uchaguzi gani usiokuwa na tume ya uchaguzi wala sheria za uchaguzi?
3. Je suala la kugombea madaraka na kuacha kumzika Mtume ndio uislamu uliotukaka wa watu hawa?
4. Kwa nini wagombee ukhalifa, hivi yawezekana kuwa Mtume alikufa bila kumteua kiongozi?
5. Kama Mtume alimteua kiongozi uchaguzi huu ulikuwa wa nini?
6. Kwa kuwa Mashia tunaamini kuwa Mtume alimteua Imam Ally kuwa khalifa wa kwanza baada yake, huoni kuwa watu hawa waliogombea uongozi walifanya mapinduzi dhidi ya serikali halali ya Mtume na khalifa wake kipenzi?
7. Kwa nini watu hawa wanaodaiwa kuwa walikuwa wacha Mungu wampiga bint pekee wa Mtume na kumuua?
8. Hivi Mtume alifurahia kitendo chao?
9. Kama ungekuwa wewe ndio Mtume ungewafurahia watu hawa waliomuua mtoto wako?
Comments
Post a Comment