ABUBAKAR NA UMARI HAWAKUMZIKA MTUME

ABUBAKAR NA UMARI HAWAKUMZIKA MTUME

Abubakar na Umar na wengi wa Maansar hawakushiriki mazishi ya Mtume kwa sababu ya mzozo wao wa kugombea ukhalifa. Kila mmoja akiamini kuwa yeye ndiye aliyestahili kuwa khalifa kana kwamba Mtume alifariki bila kumchagua mrithi wake.
Tazama: Kanzul Ummal J.5 Uk. 652

Wakati wote huo Imam Ali yuko nyumbani kwa Mtume (s.a.w.) akishughulikia maandalizi ya kumzika Mtume. Kisha baada ya kumzika Mtume (s.a.w.) Imam Ali alibaki nyumbani kwake yeye na mkewe Mwana Fatima (a.s.) wakawa wanakusanyika hapo Bani Hashim.
Abubakr baada ya kutawalishwa alimpeleka Umar bnil Khattab nyumbani kwa Mwana Fatima (a.s.) ili akawatoe wote waende kumbai Abubakr akamwagiza kuwa: Endapo watakataa kwenda kumbai, awauwe.
Umar akaenda na kijinga cha moto, Mwana Fatima alipomuona mlangoni na kijinga hicho akamuuliza: Ewe Umar! Umekuja iwasha nyumba yetu? Umar akajibu Ndiyo Wallahi nitakuunguzeni au mtoke kwenda kumbai Abubakr".
Inasemekana kuwa: Umar alipoingia nyumbani kwa Mwana Fatima, alimpiga ngumi ya tumboni, ngumi ambayo iliumiza ujauzito na kuzaliwa mtoto aliyekufa! Na kwa sababu ya kipigo hicho, afya ya Mwana Fatima ilidhoofu sana na baadaye kufariki. Umar alikuwa akiyakumbuka haya, mwenyewe husema "Laiti ningelikuwa kondoo niliyefugwa, nikanenepeshwa kiasi cha kupendeza. Akija mgeni nikatwekatwe sehemu nyama yangu ikaangwe na sehemu ibanikwe, kisha wanile na wanitoe nikiwa mavi nisiwe binadamu".
Tazama:
Kanzul Ummal J.12 Uk. 619

Tafakari haya:
1. Je Ukhalifa unapatikanana kwa kugombania na kuzozana kama walivyofanya akina Umar?
2. Ukisema ni uchaguzi, uchaguzi gani usiokuwa na tume ya uchaguzi wala sheria za uchaguzi?
3. Je suala la kugombea madaraka na kuacha kuzika Mtume ndio uislamu uliotukaka wa watu hawa?
4. Kwa nini wagombee ukhalifa, hivi yawezekana kuwa Mtume alikufa bila kumteua kiongozi?
5. Kama Mtume alimteua kiongozi uchaguzi huu ulikuwa wa nini?
6. Kwa kuwa Mashia tunaamini kuwa Mtume alimteua Imam Ally kuwa khalifa wa kwanza baada yake, huoni kuwa watu hawa waliogombea uongozi walifanya mapinduzi dhidi ya serikali halali ya Mtume na khalifa wake kipenzi?


7. Hivi alichokifanya Umar dhidi ya bint wa Mtume yaani kumpiga kiasi cha kusababisha kifo chake ndio heshima kwa Mtume wetu?

Comments