ALIPOKUFA MTUME, OMARY ALIWAZUIA WATU KUTANGAZA KIFO
HICHO
Amesema Mwana
Aisha kuwa: "Zilipotangazwa habari za kifo cha Mtume (s.a.w.) Umar bin
Khattab na Mughira bin Shuuba waliingia ndani alikolazwa Mtume (s.a.w.). Umar
akasema: Oh msiba mzito kwa kuondokewa na Mtume, kisha walitoka nje, walipokuwa
mlangoni Mughira akasema: Ewe Umar! Kwa kweli Mtume amekufa, Umar akajibu: Wewe
muongo, Mtume hajafa isipokuwa wewe ni mtu unayesumbuliwa na fitina. Mtume
hatakufa mpaka wanafiki wamalizike wote.
Tazama: Albidayatu Wannihaya J.5 Uk. 212
Hatimaye Umar alikamata upanga akaonya kuwa: Yeyote
atakayesema kuwa Mtume amekufa atakata kichwa chake. Alipofika Abubakr, Umar
akanyamaza na akaweka upanga wake chini. Kisha Abubakar akatangaza kuwa Mtume
amekufa, na hapo ndipo alipoondoka yeye na Umar kwenda mwenye ukumbi wa Bani Saida.
Huko walijumuika na Masahaba kutoka Ansar wa Madina tayari kwa uchaguzi.
Abubakr alitoa hutuba ndefu katika mkutano huo akiwakumbusha kuwa wao (Muhajir)
ndio wenye haki ya kushika uongozi mahala pa Mtume (s.a.w.).
Hutuba ambayo ilijibiwa baadaye na Hubab bin Mundhir
katika Ansar, naye akionyesha kuwa ma-Ansar wanayo haki zaidi yao, kwa sababu
kwao (Madina) ndiko kuliko shamiri na kukomaa nguvu za Uislam, na Waislamu
kupata Uhuru wa kuabudu, na ikiwa hapana budi basi kwa Muhajir atoke mmoja na
kwa Ansar atoke mmoja.
Hapo ndipo Umar aliposimama akasema: "Hilo
haliwezekani, panga mbili hazikai katika ala moja, Wallahi Waarabu hawakubali
kuwatawalisheni na hali Mtume wao hatokani na nyinyi".
Baada ya mabishano makali na kushutumiana, karibu wauwane, hatimae Abubakr akachaguliwa. Kama asemavyo Umar: "Kuchaguliwa kwa Abubakr kulitokea ghafla, Mwenyezi Mungu alizuia shari zake, na atakaerejesha kitendo kama hiki auliwe".
Baada ya mabishano makali na kushutumiana, karibu wauwane, hatimae Abubakr akachaguliwa. Kama asemavyo Umar: "Kuchaguliwa kwa Abubakr kulitokea ghafla, Mwenyezi Mungu alizuia shari zake, na atakaerejesha kitendo kama hiki auliwe".
Tazama:
Tarikhul Tabari Juzu 2 Uk. 446 na 457
Tarikh Ibn Athir Juzu 2 Uk. 223
Sahih Bukhar Juzu 8 Uk. 210
Albidayatu Wannihaya Juzu 5 Uk. 215
Abubakr na Umar hawakuwahi kumzika Mtume (s.a.w.).
Tazama: Kanzul Ummal J.5 Uk. 652
Tazama: Kanzul Ummal J.5 Uk. 652
Tafakari haya:
1.
Je Ukhalifa unapatikanana
kwa kugombania na kuzozana kama walivyofanya akina Umar?
2.
Ukisema ni uchaguzi,
uchaguzi gani usiokuwa na tume ya uchaguzi wala sheria za uchaguzi?
3.
Je suala la kugombea
madaraka na kuacha kuzika Mtume ndio uislamu uliotukaka wa watu hawa?
4.
Kwa nini wagombee
ukhalifa, hivi yawezekana kuwa Mtume alikufa bila kumteua kiongozi?
5.
Kama Mtume alimteua
kiongozi uchaguzi huu ulikuwa wa nini?
6.
Kwa kuwa Mashia tunaamini
kuwa Mtume alimteua Imam Ally kuwa khalifa wa kwanza baada yake, huoni kuwa
watu hawa waliogombea uongozi walifanya mapinduzi dhidi ya serikali halali ya
Mtume na khalifa wake kipenzi?
Comments
Post a Comment