IMAM ALI (a.s) ALIUPINGA UKHALIFA BANDIA WA ABUBAKAR
Mwana Aisha amesema kuwa:- "Ali (a.s.) hakumbai Abubakr ila baada ya miezi sita kupita".
Abubakr alikwenda nyumbani kwa Imam Ali (a.s) akawakuta Bani Hashimu wamekusanyika, Imam Ali akamwambia "Sisi haikutuzuilia kukukubali ewe Abubakr, kwa kupinga heshima yako wala ubora aliokupa Mwenyezi Mungu, lakini sisi tunaamini kuwa jambo hili (la uongozi) ni letu na nyinyi mmelipokonya kwetu".
Kisha akawa anamtajia nafasi aliyonayo kwa Mtume (s.a.w.) na haki zake mpaka Abubakr akaangua kilio.
Taz: Tarikhut Tabari J. 2 Uk. 448
Huo ndio ukweli, na sisi Mashia tunafuata nyayo za imamu wetu kuupinga ukhalifa bandia wa Abubakar, Umar na Uthuman.
Comments
Post a Comment