LENGO LA KUSOMA SIRA (HISTORIA YA UISLAMU):

LENGO LA KUSOMA SIRA (HISTORIA YA UISLAMU):

Hakika kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu na kizazi chake kitakasifu ni kufuata njia iliyonyooka inayofikisha kwenye wema na ushindi kwa sababu ni njia inayokuepusha na upotovu na ghadhabu za Mwenyezi Mungu8.

Na ndio njia ya manabii ambao Mwenyezi Mungu aliwaneemesha kwa neema ya uongofu wake unaowapeleka kwenye haki. Ndiyo maana akaamrisha kuwafuata, Mwenyezi Mungu akasema: “Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza, basi fuata mwongozo wao.”9

Pia kwa ajili hiyo ndiyo maana sira ya yule hitimisho la manabii na sira ya mawasii wake watakasifu imekuwa ni chanzo kati ya vyanzo vya sheria ya kiislamu, na ni chemchemu ya maarifa na elimu ya kiislamu na ni sawa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu cha milele, kama ilivyoelezea kuhusu hilo Hadithi ya vizito viwili iliyo mutawatir.

Kama hujaisoma sira ya viongozi hawa watakatifu itakuwa vigumu huijua na kuifuata. Hivyo kutokusoma sira ni sawa na kujipoteza njia mwenyewe.

Rejea:
8. Al-Fatiha: 5 – 7.
9. Al-An’aam: 90.

Zaidi ya hapo ni kuwa sira yao - Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao wote kwa ujumla - ina faida kubwa katika kufahamu makusudio ya Kitabu kitakatifu na tafsiri ya Aya zake tukufu.

Pia sira yao hutubainishia jinsi ya kutekeleza mafunzo juu ya kiislamu katika maisha ya mwanadamu anayeishi katika maisha haya. Kwa hiyo tunafahamu kuwa kusoma sira yao kwa namna sahihi kutatupa silabasi muhimu katika malezi ya kiislamu na njia sahihi ya kujifunza mwenendo sahihi katika maisha.

Comments