MAANA YA USHI‘A KUTOKA VITABU VYA SUNNI
Maana ya Ushi‘a Neno Shi‘a (شيعة) limetokana na neno la Kiarabu at-tashayyu (التشيع) lenye maana ya kufuata. Kulingana na al-Qamus na Lisanu ’l-‘Arab, marafiki na wafuasi wa mtu wanaitwa Shi‘a wake. Kulingana na Taju ’l- ‘urus, kikundi cha watu wanoafikiana juu ya jambo (lolote) wanaweza kuitwa “Shi‘a.” Neno hili hutumika sawa sawa kwa umoja na wingi, vile vile hutumika sawa sawa kwa wanaume na wanawake.
Katika Qur’ani imetumiwa kwa wafuasi wa Mitume wa Allah (s.w.t.)
(a) Katika kisa cha Musa (a.s.) inasema hivi: Huyu ni katika Shi‘a wake na yule ni katika adui zake, yule ambae alikuwa Shi‘a wake alimuomba msaada juu ya yule adui yake. 2
(b) Katika kisa cha Nuh (a.s.) inasema hivi:- Na hakika Ibrahim alikuwa katika kundi (Shi‘a) lake (Nuhu).3
Kamusi za Kiarabu baada ya kutoa maana ya kawaida ya neno Shi‘a, kwa kawaida huongeza: “Jina hili kijumla hutumika kwa wale wenye mapenzi na kumfuata Ali (a.s.) na watu wa nyumbani kwake, na imekuwa ndio jina lao makhsusi”.4
Rejea:
2. Qur’ani 28:15
3 Qur’ani 37:83
4 Al-Qamus, Juzuu ya 2;
at-Turayhi, Majma‘ul ’l-Bahrayn, Juzuu ya 2 uk. 539;
Ibn al-Athir al-Jazari, an-Nihayah, toleo la Misri, [1383/1963], Juzuu ya 2 uk. 519-520.
Shaykh al-Mufid (aliyekufa 413 A.H. / 1022 M.) ameeleza kwamba wakati neno Shi‘a linapotumika na Sarufi yenye kuainisha ‘al’ (al-Shi‘a) basi ina maana ya “kundi pekee lenye kumfuata Imam Ali (a.s.) kwa mapenzi na imani (itikadi) na kwamba alikuwa ni Imamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) bila mwonya wowote....”5
Kwa ufupi, Shi‘a wamepata jina hili kwa sababu wanamfuata Imam Ali (a.s.) na kizazi chake Maasumin, na kupuuza madai ya watu wengine ya Uimamu. Ni Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe aliyewapa jina hili wafuasi wa Ali (a.s.).
Rejea:
5 al-Mufid, Shaykh, Awa’ilu ’l-Maqalat (Qum: Toleo la 2, 1370 A.H.) uk. 2-3.
Comments
Post a Comment