MAHUSIANO KATI YA HISTORIA YA UISLAMU NA SIRA
Historia:
Historia ni mkusanyiko wa matukio na uzoefu wa wanadamu waliopita ukilinganisha na zama tunazoishi hivi sasa.
Historia ya Uislamu:
Hakika historia ya Uislamu ni historia ya dini ya milele ya kiislamu, tangu ulipodhihiri, kuenea kwake na harakati zake katika maisha. Pia inakusanya historia ya walioibeba dini na kuihami ambao walikesha wakihudumia na kulinda dini dhidi ya vitimbi vya maadui wake.

Hivyo hakika sira ya bwana wa mitume na sira ya kizazi chake kitakasifu ambacho kilipewa jukumu la kufikisha dini, kutekeleza na kuilinda, inakuwa ni sehemu isiyogawika ndani ya historia yenyewe ya Uislamu (yaani ndio historia yenyewe ya Uislamu).
Kwa sababu wao walizama ndani ya Uislamu na wakaihami sheria, wakatoa nafsi zao na maisha yao kwa ajili ya Uislamu. Hivyo misimamo yao ya kidini ndio Uislamu wenyewe na harakati zao ndio harakati za Uislamu wenyewe. Wao hudhihirisha kimatendo mafunzo halisi ya Uislamu na huyaelezea maelezo halisi. Hivyo historia yao
ndio historia ya Uislamu katika hatua zake zote na mambo yake yote, wala siyo historia ya mtu fulani kati ya waislamu.
ndio historia ya Uislamu katika hatua zake zote na mambo yake yote, wala siyo historia ya mtu fulani kati ya waislamu.
Comments
Post a Comment