MATENDO YALIYO HARAMU KWA MUISLAMU {3}
1. Kupoteza haki:
Hapa kuna maana nyingi, kuna haki za Mwenyezi Mungu, haki za Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} na haki za Waislamu kwa wenzao. Pia kuna haki ya mwanadamu kwa mwingine. Zote hizo ukipoteza moja wapo ni dhambi.
2. Kuiba:
Ni dhambi ambayo inajulikana pote ulimwenguni. Mwenyezi Mungu amesema: 'Na mwizi mwanamume na mwizi mwanamke, ikateni mikono yao, malipo ya yale waliyo yachuma. Ndio adhabu itokayo kwa Mwenyezi Mungu." {Qur'an Sura ya 5 aya ya38}.
3. Ukuwadi na kusaidia katika mambo ya ndoa hata kwa mke wake:
Mtukufu Mtume {s.a.w.w} amesema: "Hataingia peponi DAY-YUSI wala hapati harufu ya peponi." Akaulizwa, "Ni nani huyo?
Akasema, "Yule mume ambaye anajua vema kwamba mke wake analala na mwanamume mwingine {na haoni aibu}.
4. Kusema uwongo:
Ni haramu, dhambi kubwa sana. Amesema Imam Al-Baqir {a.s.}: "Hakika Mwenyezi Mungu ameweka kwa kila shari {uovu} kufuli na ufunguo wa makufuli hayo ni ulevi, na uwongo ni ubaya zaidi kuliko ulevi."
5. Kuteta na kufitinisha:
Mwenyezi Mungu amesema: "Wala baadhi yenu wasiwaseme wengine. Je! Mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa?" {Qur'an, Sura ya 49 aya ya 12}.
Mtukufu Mtume {s.a.w.w} amesema: "Hataingia peponi mfitini {mwenye kutangaza maneno ya huyu kwa yule ili atie fitina na kuwagombanisha}."
6. Kula riba:
Mwenyezi Mungu amesema:"Wale wanao kula riba................ wakasema, 'Biashara na ni kama riba.' Hali Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba." {Qur'an, Sura ya 2, aya ya 275}.
Mtukufu Mtume {s.a.w.w.} amesema: "Mwenyezi Mungu amemlaani mla riba, mtoa riba, na mwandikaji wa riba na mshuhudiliaji hayo.''
7. Kuua:
Mwenyezi Mungu amesema:' Na mwenye kumuua Muislamu kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu, humo atakaa milele, na Mwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani na amemwandalia adhabu kubwa." {Qur'an Sura ya 4 aya ya 93}.
8. Hiyana:
Mwenyezi Mungu amesema: "Hakika, Mwenyezi Mungu hawapendi wafanyao hiyana. {Qur'an, Sura ya 8, aya ya 58}
9. Dhuluma:
Mwenyezi Mungu amesema: "Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafirika na{haya} wanayoyafanya madhalimu. Hakika yeye anawaakhirisha tu mpaka siku ambayo macho {yao} yatakodolea {yatoke nje kwa khofu}." {Qur'an, Sura ya 14 aya ya 42).
Comments
Post a Comment