QUR’AN INASEMAJE KUHUSU BAADHI YA WAKRISTO

QUR’AN INASEMAJE KUHUSU BAADHI YA WAKRISTO

Allah (s.w) anasema kuwa, “kwa hakika utakuta maadui wakubwa wa waumini ni wayahudi na wapagani, na utakuta kuwa marafiki wa waumini ni wale wanasema kuwa sisi ni wakristo. Hiyo ni kwa sababu miongoni mwao kuwa makasisi na watawa. Na wanaposikia ujumbe ulioteremshwa na Mtume, utawaona wanabubujikwa na machozi kwa kuuona ukweli. Ndipo watasema, ewe Mungu wetu, tumeamini, kwa hiyo tuweke pamoja na wakweli. Kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na ukweli uliokuja kwetu, ili Mola wetu atuweke moja na watu wa haki? Kwa hiyo Allah amewalipa kwa hayo wanayoyasema, pepo (mabustani) inayobubukwa na mito, wakae humo milele. Hayo ndio malipo ya wafanya mema. 5:82-85”

Kisha Allah anasema, “kisha tuliwatumia mitume ili wafuate nyayo zao, na tukamtuma Yesu baadaye na tukampa injil na tukaweka huruma na uvumilivu katika nyoyo za wafuasi wake. Wao walibuni utawa ambao hatukuwaagiza. Sisi tuliwaagiza kufuata maelekezo ya Mwenyezi Mungu, lakini hawakulizingatia hili. Hivyo tuliwalipa waaminio miongoni mwao kwa malipo, lakini wengi wao wamevuka mipaka (57:27).

Japokuwa Allah amewakosoa wakristo kwa kuvuka mipaka na kuzidisha mambo ambayo hawakuwa wameamrishwa na yeye, lakini amewasifu vya kutosha kwa kuwa wenye msaada kwa Uislamu na waislamu.

Ukirudi katika historia utawakuta wakristo waliopambana na kuuawa wakimtetea Mtume Muhammad na familia yake. Na kwa kufanya hivyo waliutetea Uislamu kwa sababu hawa ndio viongozi wa Uislamu japokuwa wanafiki na makafiri waliwachukia sana na kuendesha vita dhidi yao.


Walioendesha vita dhidi ya Ahlulbayt, mifano yao ni wafuatao, Abubakar bin Quhafa, Umar bin Affan, Yazid bin Muawiyyah, Aisha bint Abubakar, Twalha, Zuberi, Abdurahman bin Auf, Muawiya bin Abi Sufian, Yazid bin Muawiya, Hindu mama wa Muawiyah, Abdillah bin Ziyad, n.k. hawa ndio watu walioendesha operesheni ya kuwatetekeza Ahlulbayt, kila mmoja alifanya mauaji wakati wa zama zake kwa namna aliyojisikia mwenyewe. 

Comments