BADALA YA KUMUOMBA ALLAH MOJA KWA MOJA, KWA NINI TUOMBE VISABABISHO?”

BADALA YA KUMUOMBA ALLAH MOJA KWA MOJA, KWA NINI TUOMBE VISABABISHO?”

Matarajio yetu ya kudumu kuhusu haja zetu, dhiki, na hofu yamewekwa juu ya Allah, Mkamilifu. Lakini Qur’an Tukufu inasema yatupasa kumfikia Allah, kupitia baadhi ya njia (visababisho) za kupelekea.

“Enyi ambao mmeamini! Mcheni Allah na tafuteni njia ya kumfikia Yeye…” (5:35).

Dhuria Watukufu Wa Muhammad Ni Njia (Wasyla – Visababisho) ya Neema Za Mungu. Sisi Shi’a hatuwachukulii kizazi cha Mtume kama ufumbuzi wa matatizo yetu yote. Tunawaona wao kama wacha Mungu zaidi katika waja wa Allah na kama njia za neema za Mungu. Tunajiambatanisha wenyewe kwenye ile familia bora zaidi kwa mujibu wa maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Katika hadith nyingi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), amependekeza kwetu, kwamba katika shida zetu tuwaombe watoto wake kama njia ya kumfikia Allah. Wengi wa Maulamaa wa kisunni, kama Hafiz Abu Nu’aimi Isfahani katika kitabu chake “Nuzulu’l-Qur’ani fi Ali” (Ufunuo katika Qur’ani kuhusu Ali), Hafiz Abu Bakr Shiraz katika kitabu chake “Ma Nazala mina’l-Qur’an fi Ali” na Imam Ahmad Tha’labi katika Tafsir (Sharhe) yake anasema kwamba Wasilat (njia ya kumfikia) katika aya hiyo hapo juu ina maana ya watoto wa Mtume (s.a.w.w.).

Maneno haya yamekuwa wazi kwenye hadith nyingi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Abi’l- Hadid Mutazali, mmoja wa Mualamaa maarufu wa kisunni, anasema katika “Sherhe Nahjul’l- Balagha” yake, Juz. 4, Uk, 79, kwamba Bibi Fatima Zahra, alitaja maana ya maneno ya Aya hii mbele ya Muhajirina na Ansari, wakati anatoa khutuba yake yenye kuhusu kunyang’anywa shamba lake la Fadak.
katika maneno haya: “Namshukuru Allah Ambaye kwamba Ukuu Wake na Nuru Yake, Wakazi wa mbinguni na ardhini hutafuta njia ya kumfika Yeye. Miongoni mwa viumbe Wake sisi ni njia (Wasilat) ya kumfikia Yeye.”

Miongoni mwa hoja zetu nyingi zinazokubaliwa kuhusu uhalali wa kufuata kwetu kizazi cha Mtume ni “Hadith ath-Thaqalain” - vizito viwili, ambayo usahihi wake umekubaliwa na Madhehebu zote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama mtashikamana na viwili hivi, kamwe, hamtapotea baada yangu.”

Huu ndio ukweli wa Ushia, na mtu akiwa Mshia anakuwa ameukamata Uislamu barabara na hatohuzunika milele kwa sababu yuko pamoja na Mtume Muhammad na Ahlulbayt wake (a.s).

Comments