MALEZI YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)
Ingawaje nchi ya Arabu haikuwa na serikali yoyote ya
kitaifa, kijimbo au kienyeji, jiji la Makka lilikuwa linatawaliwa na kabila la
Qurayishi.
Kabila la Qurayish lilikuwa na koo kumi na mbili. Koo
hizi zilishirikiana majukumu ya kudumisha kiasi kidogo cha sheria na utulivu
katika mji wa Makka. Moja ya koo za kabila la Qurayshi ilikuwa Bani Hashim.
Kila ukoo ulikuwa na kiongozi wake. Kiongozi wa Bani Hashim alikuwa Abu Talib
bin Abdul Muttalib bin Hashim bin Abd Manaf bin Qusayy. Kama walivyokuwa babu
zake, Abu Talib pia alikuwa mfanyabiashara. Zaidi ya kuwa mkuu wa ukoo, alikuwa
pia mlezi wa Al-Kaaba - Nyumba ya Mwenyezi Mungu - iliyojengwa Makka, karne
nyingi zilizopita, na Mtume Ibrahim na Ismaili na wakaitoa wakfu imtumikie
Mwenyezi Mungu.
Abu Talib alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Abdullah. Mwaka wa 570 A.D., Abdullah alikwenda Syria na msafara wa biashara. Miezi michache kabla hajasafiri kwenda Syria alimuoa Amina binti Wahab, mwanamke kutoka Yathrib (Madina). Wakati Abdullah alipokuwa anarudi kutoka Syria, aliugua na kufa. Alikuwa na umri wa miaka 17 tu alipokufa. Alipoondoka Makka, mke wake alikuwa mja mzito na alikuwa anaishi nyumbani kwa shemeji yake, Abu Talib. Miezi miwili baada ya kifo cha Abdullah, alijifungua mtoto wa kiume. Babu wa mtoto huyu, Abdul Muttalib, alimpa jina la Muhammad. Muhammad alizaliwa tarehe 8, Juni, 570, nyumbani kwa baba yake mdogo, Abu Talib mjini Makka.
Siku za usoni, mtoto mchanga Muhammed alikuwa ateuliwe na Mwenyezi Mungu (s.w.t) kuwa Mjumbe Wake wa dunia yote, na alikuwa abadilishe majaliwa na historia ya binadamu daima milele. Muhammad alikuwa na umri wa miaka sita wakati mama yake, Amina binti Wahab, alipokufa baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kutokana na kifo chake hicho, babu yake Muhammad (S.A.W.W),
Abdul Muttalib, alimchukua ili amlee nyumbani kwake. Lakini ilikuwa baada ya
miaka miwili tu Abdul Muttalib naye alifariki. Abdul Muttalib alikuwa na watoto
wa kiume kumi. Alipokaribia kufa, aliwaita watoto wake wote, na alimteuwa
mwanae Abu Talib kama mkuu mpya wa ukoo wa Bani Hashim. Pia alimfanya mlezi wa
Muhammad (S.A.W.W).
Wote wawili Abu Talib na Abdullah, baba wa Muhammad,
walikuwa watoto wa mama mmoja, ambapo watoto wengine wa Abdul Muttalib
walizaliwa na wakeze wengine. Abu Talib alimpeleka Muhammad nyumbani kwake.
Muhammad aliwashinda wote (kwa tabia).
Abu Talib na mkewe (Fatuma bint Asad) walimpa Muhammad
mapenzi makubwa sana. Walimpenda zaidi kuliko walivyowapenda watoto wao.
Muhammad alizaliwa ndani ya nyumba yao. Kuzaliwa kwa Muhammad ndani ya nyumba
hiyo kulisababisha nyumba hiyo iwe na neema nyingi; na sasa baada ya kifo cha
Abdul Muttalib, alirudi tena ndani ya nyumba hiyo.
Muhammad alipokuwa mtoto, hakuonyesha kuvutiwa na
mwanasesere na michezo ya watoto. Katika ujana wake, hakuonyesha kupenda
michezo na burudani, au kuwa katika makundi ya vijana wa rika lake. Pamoja na
kwamba alikuwa kijana, alipendelea zaidi upweke kuliko kuchanganyika kwenye
makundi ya vijana wenzake.
Comments
Post a Comment