UFALME NA USULTAN NI KINYUME CHA UISLAMU
Mwenyezi Mungu Mwenye Rehma amesema katika Qur’ani tukufu kuwa: “Hakika wafalme wanapouingia mji, wanauharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili; hivyo ndivyo wanavyofanya”. (27:34)
Aya hii inatoa ujumbe kwa Waislamu ulio muhimu sana. Inaeleza kwamba unapotokea ufalme usiotosheka na milki yake na ukawa na nia ya kutaka kupanua himaya yake na mipaka yake, basi daima ufalme kama huu hauwezi kuzingatia kanuni za haki katika nidhamu yake. Na hapo ufalme huo hupotoka na kuanza kuvamia nchi nyingine na kuiteka miji yake na kufanya ufisadi ikiwa ni pamoja na kuharibu mali na kuhilikisha maisha ya wanadamu. Kwa kuwa Mawahhabi historia yao inaonyesha kutokana kwao na mambo ya ufalme na mauaji hapana shaka kuwa aya hii inazungumzika katika fitna yao.
Fitina za wafalme zilithibiti pale ambapo Abubakar alipopora madaraka toka kwa imam Ally (a.s) akaagiza wauawe mara moja Mashia waliogoma kulipa zaka kwa sababu ya kutoutambua utawala wake batili.
Tukio hili liliendelezwa na Muawiyah pale alipowahonga watu wawe dhidi ya Imam Ally (a.s) na pia kuajili watu ambao kazi zao zilikuwa kuwatafuta wafuasi wa imam Ally na watu wote wanaoupinga utawala wake na kulisha sumu na kuwaua mara moja. Miongoni mwa waathirika wa mpango huu ni imam na khalifa wetu wa pili yaani imam Hassan bin Ally (a.s).
Mfalme mwingine hatari anayethibitisha aya hii ni Yazid bin Muawiyah ambaye aliongoza vikosi vyake na kuuvamia mji wa Makkah na kuwaua waislamu mia saba na kuwabaka wanawake zaidi ya elfu tatu. Kilele cha udhalimu wake ni pale alipoifyeka familia ya Mtume wetu katika eneo la karbala, hapo aliwaua watu 72 akawemo kiongozi wa ukoo huu na pia imam wetu wa tatu yaani imam Hussein bin Ally (a.s).
Mifano ni mingi lakini tumalizie kwa kumtaja mfalme Muhammad AlSuud na kibaraka wake yaani Sheikh Muhammad Abdul wahhabi ambao walitengeneza ushirika chini ya msaada ya Uingereza wakaanzisha Uwahhabi. Kundi ambalo limekwisha ua waislamu malaki kwa mamilioni katika dunia nzima. Na leo hii limetapakaa kila kona ya dunia kwa majina kama vile Answari Sunnah, Salafi swaleh na dini kamili.
Watu hawa katika zama za leo wanashirikiana na mashirika ya kijasusi ya Israel na Marekani katika kuuhujumu Uislamu. Utakuta asilimia tisini na tisa ya watu wanaowachinja ni waislamu kwa kuwatuhumu kwa hoja za uongo. Makundi maarufu ya mauaji yanayoendeshwa na Mawahhabi ni Taliban, Alqaida, Boko Haram, Answar diin, Answar Shariah, Alshabab, Jabhat Annusra, ISIS, ISIL na Ahrar Sham, na mengineyo.
Comments
Post a Comment