ASILI YA UISLAMU
Uislamu ni dini ya
kimaumbile ya mwanadamu iliyoandaliwa na Muumba ili dini hii tukufu iwaongoze
wanadamu wote. Msingi wake mkuu ni tawhid yaani Umoja wa Mungu.
Katika Uislamu watu
wanatakiwa kuchagua aidha wafuata muongozo wa Uislamu (Qur’an) au waende
kinyume chake. Ukiufuata muongozo Allah atakulipa kheri na ukiupinga muongozo
Allah atakuadhibu kwa kukuingiza Jahanam.
Mwenyezi Mungu aliueneza
Mfumo huu kupitia mitume wake. Mtume wake wa kwanza alikuwa nabii Adam na Mtume
wake wa mwisho ni Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Allah alituma mitume wengi
kuongoza watu kutokana na tabia mbaya waliyonayo wanadamu, pindi tu Mtume
anapoondoka au kufariki dunia, wafuasi wake hurtadi dini na kufuata mifumo
batili ya maisha. Mfano ni pale Nabii Mussa alipokwenda mlimani kupokea amri za
Allah kwa siku thalathini tu, aliwakuta masahaba wake wamekwisha tengeneza
sanamu na kuliabudu.
Kipindi cha uhai wa Mtume
Muhammad (s.aw.w), Uislamu ulikuwa mfumo wa mawazo ya aina moja tu. Mara tu
alipofariki, ufa wa kwanza ulijitokeza katika ile “nguzo imara” ya Uislamu.
Wafuasi wake – Waislamu – walikingamizwa kwenye makundi mawili. Katika
kingamizo hili, wengi wa maswahaba zake walikuwa upande mmoja na watu wa
nyumbani kwake (Ahlulbayt) kwa upande mwingine. Wakati watu wa nyumbani kwake
wakiwa wameshughulishwa na mazishi yake, baadhi ya maswahaba zake
walishughulika katika “kuchagua” kiongozi mpya wa kumrithi Mtume.
Katika ule mwanya kati ya
kifo na mazishi yake, hili kundi la mwisho (la maswahaba) lilijikusanya katika
banda la Saqifah hapo Madina, na likamchagua mmoja (Abubakar) kati yao wenyewe
kama mkuu mpya wa umma wa Waislamu. Wao, kisha wakawakabili watu wa ile familia
iliyoondokewa kwa jambo lililokwisha fanywa na kuthibitishwa. Mkabiliano huu,
kwa bahati mbaya sana, ukawa Sura ya kudumu ya historia ya Waislamu.
Muhammad, Mtume wa Allah
(s.w.t,), Rehma na amani juu yake na juu ya Ahlul-Bayt wake, alitokana na ukoo
wa Bani Hashim. Baada ya kifo chake mwaka 632 A.D., binamu yake, mkwe wake na
mrithi mstahiki wake, Ali ibn Abi Talib, alimfuatia yeye kama mkuu mpya wa Bani
Hashim. Wengi wa maswahaba wa Muhammad, Mtume wa Uislamu, walikuwa wamelea
uadui wa siri juu yake.
Hawakuweza kumuonyesha uadui
wao wakati wa uhai wake Mtume lakini mara walipokuwa na amri juu ya serikali
yake hapo Madina, walikuwa wameazimia, kutoiachia, kwa kukosea kwa namna yoyote
ile, iangukie kwenye mikono ya Ali ibn Abi Talib.
Watu wa nyumba ya Muhammad,
Mtume wa Allah (s.w.t.) hivyo walizuiwa, kwa nguvu kubwa ya wanadamu, sio tu
kwenye urithi wa moja kwa moja bali pia kwenye nafasi zote za mamlaka na
madaraka katika serikali za wafuasi wake zilizofuatia.
Marafiki, wafuasi na
wanaounga mkono nyumba ya Muhammad Mustafa, Mtume wa Allah (s.w.t.) wamekuwa
kihistoria wakiitwa Shia; na marafiki, wafuasi na wanaowaunga mkono maswahaba,
yaani, lile kundi lililofanikiwa kutwaa madaraka hapo Madina, limekuwa likiitwa
Sunni. Nitayatofautisha pia makundi haya mawili kwa majina haya.
M. Shibli, mwanahistoria
mashuhuri wa Kihindi wa Uislamu, anasema kwamba takriban historia zote za
Uislamu zimeandikwa na wanahistoria wa Sunni. Kauli hii inamaanisha kwamba
wanazuoni wa Shia hawakuandika historia yoyote ya Uislamu. Kwa nini
hawakuandika? Hawakuandika historia kwa sababu ya wazi. Makhalifa wote,
masultani na wafalme, wote walikuwa Sunni.
Aliyekuwa Shia hakuruhusiwa
kuchapisha ufafanuzi wa historia ya Kiislamu ambao ulikuwa unatofautiana na ule
ufafanuzi wa kiserikali, na hakuwa na haja ya kuendeleza kile alichoamini kuwa
ni upotoshaji wa ukweli. Yeye, kwa hiyo, aliamua kutoandika historia yoyote
kabisa.
Kwa namna hii, yalikuwa ni
yale “maelezo” ya kiserikali ya historia ya siku za mwanzo za Uislamu ambayo
yalipata kuenea na yakapata kukubalika. Lilikuwa ni jambo la kimantiki kabisa
la kufanya kwa serikali za karne za mwanzoni za Uislamu kuingiza kwenye
mzunguko, ile hekaya tu, ambayo ilikuwa inakubaliana na itikadi ya kundi lao.
Ilikuwa pia na mantiki
kabisa kwa wafuasi wa sera za serikali hizo tunazozizungumzia, kutii itikadi
hiyo. Na katika kutii itikadi hiyo ya kundi, kama walihisi kwamba ni muhimu
kufunika ukweli, au kwa kiwango chochote, kufunika ule upande mwingine wa
Hadith hiyo, ilikuwa na mantiki kabisa kufanya hivyo.
Hakuna jambo lolote la
ajabu, la kushangaza au kushitusha katika mwenendo wa wanahistoria wa Sunni.
Kitu chenye mantiki kabisa kwao kukifanya kilikuwa, na bado ni, kutetea uhalali
wa matukio ambayo yalitukia ndani ya Saqifah, ambamo baadhi ya maswahaba,
katika shambulizi la kuwahi kabla ya wengine, walitwaa serikali ya Muhammad,
kiongozi wa Arabia.
Kile ambacho hata hivyo ni
cha kushangaza na cha kushitusha, ni kwamba wanahistoria wa kimagharibi, yaani,
wale Mustashriq, wamemeza, kama jambo la kweli kabisa, kila ambalo wanahistoria
wa “baraza” la Kiislamu limewachotea wao kama “ukweli.” Hawa Mustashriq
wanadhaniwa kwamba hawana upendeleo, sio wafuasi, na wasiohusika kwa jazba kwa
hali yoyote ile. Matokeo ya mashindano fulani katika zama za kale za Uislamu,
kwa njia moja au nyingine, yasingeweza kuleta tofauti yoyote kwao.
Na bado, vitabu vya wengi
wao vinaonyesha, sio ukweli bali ufafanuzi na propaganda za kundi lililokuwa
madarakani. Kwa maana hii, kazi zao ni uigaji wa vile vitabu “vilivyotiwa
msukumo” na kile Wakomunisti wanachokiita “jamii inayotawala” ya Waislamu.
Masunni licha ya serikali
kuwa chini yao bado hawaridhiki na wala hawatoridhika mpaka wawakandamize na
kuwaua wafuasi wa Mtume na Ahlulbayt wake.
Utawasikia wakitoa hadith za
uongo kuwa yaliyotokea baina ya masahaba yakaliwe kimya, yaani yasisemwe.
Maneno hayo yakwenda kinyume na Qur’an ambayo imesheheni historia za watu na
jamii mbalimbali tena ikiwataja kwa uwazi kama walikuwa wema au waovu. Kwa nini
masahaba iwe tofauti? Kwa nini tuzuiwe kuwajadili kwa uhalisia? Kama Qur’an
imewajadili masahaba wa mitume wengine bila kificho kama ni wema au waovu.
Mfano ni ule nilioutoa wa wafuasi wa nabii Mussa. Hapo ongeza wafuasi wa Nuhu
na gharika lililowabana.
Hivi watu hawa hawafikiri au
ni upofu wa mapenzi? Jiulize Uthuman aliuawa na Masahaba wenzake. Lakini
masunni wanasema tusiwajadili na kwamba wote ni wema. Hivi inawezekanaje muuaji
na aliyeuawa wote wawe sawa mbele za Allah? Huu ni upofu rohoni.
Comments
Post a Comment