IMAM ALI (AS) NA MFANYA BIASHARA
ASIYE NA HESHIMA
Imam Ali (as) wakati wa
ukhalifa wake, mara nyingi alikuwa akitembelea masoko na kuwashauri na
kuwaongoza wafanya biashara.
Siku moja, alipokuwa akipita
katika soko la tende, alimuona msichana mdogo akilia, Imam aliuliza sababu ya
machozi yake ambapo (msichana) alieleza:
“Bwana wangu alinipa dirham
moja (kwa ajili) kununulia tende. Nilizinunua (tende) kwa mfanya biashara huyu,
lakini niliporudi nyumbani, bwana wangu alizikataa. Sasa ninataka kuzirudisha
lakini mfanya biashara anakataa kuzichua.”
Imam Ali (as) alimgeukia
mfanya biashara na kumuambia, “Mtoto huyu ni mtumwa na hana mamlaka yake
mwenyewe. Chukua tende na umrudishie fedha yake.”
Mfanya biashara alisogea
mbele na huku wafanya biashara na watazamaji wengine wakimtazama, alimpiga Imam
kifuani katika jitihada za kumsukuma atoke mbele ya duka lake. Watu waliokuwa
wakishuhudia tukio hilo, walikimbia na kumuambia huyo mwanaume:
“Unafikiri unafanya nini?
Huyu ni Ali Ibn Abi Talib (as)!”
Uso wa mfanya biashara
ulipauka alipokuwa amesimama akaduwaa. Mara moja alichukua tende kutoka kwa
msichana na akamkabidhi fedha. Kisha akamgeukia Imam (as) akaomba, “Ewe Amirul
Muuminuun! Niwie radhi na nisamehe.”
Imam (as) alijibu,” Nitakuwa
radhi na wewe tu pale utakapobadili tabia yako na kuwa njema na ukajali maadili
na heshima.”
Mazingatio:
1. Imam
Ally ni kiongozi hata kama mawahhabi na vibaraka wengine wa bani Umaya
wanachukia.
2. Uongozi
ni kutumikia watu sio ufisadi wala kuuza sura
3. Kiongozi
anatakiwa ajichanganye na jamii na sio kukaa ikulu pekee na kujifanya mfalme.
Comments
Post a Comment