MAADILI
Allah Mwenye hekima Anasema
kumwambia Mtume Muhammad (s.a.w.w):
“Na hakika wewe una tabia
tukufu.” (Suratul Qalam: 4).
Mtukufu Mtume (saw) alisema:
“Nimetumwa (kama mtume) ili kuja kukamilisha maadili.”
(Jaame Al Saadaat, Juz, 1.
Uk. 23)
Uadilifu ni hali ya
kuwatendea watu matendo ambayo hata kama ungetendewa wewe ungefurahi. Tena matendo
yenye unayafanya bila ubaguzi wala upendeleo.
Kwa mwanadamu, maadili huleta
heri na fahari katika ulimwengu huu na wepesi huko Akhera. Kunyanyua hadhi ya
mtu katika ukaribu wake kwa Mwenyezi Mungu na humsaidia katika ukamilifu wa
dini yake, Mitume wote, mawalii na wateule wa Mwenyezi Mungu walikuwa na
maadili ya kupigiwa mfano, na kila mu’umini anapaswa kujipamba kwa maadili
hayo, ili mizani ya amali iwe mizito zaidi Siku ya Hukumu.
Mtukufu Mtume (saw) amesema:
“Hatima ya muda wetu ni moja, kwa yule mwenye maadili mazuri. Maadili mabaya
humfanya mtu ataabike kwa kubanwa mbavu kaburini na (adhabu ya) moto wa
jahannam (huko akhera) na ukosefu wa marafiki katika ulimwengu huu.”
Mtu hapaswi kupimwa kwa
mujibu wa maarifa yake, utajiri au cheo, bali kwa mujibu wa tabia zenye
kusifika, zinazomfanya akubalike mbele ya Allah na kwa kuwa mtukufu na msifiwa
mbele ya macho ya watu. (Taz: Tadhkirah al-Haqaaiq, uk. 57)
Ndugu zanguni katika imani
tujipe mazoezi ya uadilifu na tuepukane na tabia zote za ukatili, dhulma,
uonevu, kujikweza, kujifakharisha, husda, na kila aina ya tabia mbaya.
Comments
Post a Comment