MALALAMIKO DHIDI YA MUME
Imam Ali (a.s) katika zama za
ukhalifa wake, yeye mwenyewe alikuwa akisikiza malalamishi na manung’uniko ya
watu moja kwa moja. Katika siku za joto jingi watu hawakuweza kutoka kwenye
nyumba zao baada ya adhuhuri. Imam Ali (a.s) alikuwa akiketi nje kwenye kivuli
cha ukuta kila siku ili kama mtu yeyote alikuwa na malalamiko aweze kuonana
naye ana kwa ana. Wakati mwingine alikuwa akitembea vichochoroni na barabarani
akiangalia hali za watu zilivyo.
Siku moja alirudi kwenye makao
yake akiwa amechoka huku jasho likimtoka, na alimkuta mwanamke mmoja akimsubiri.
Mwanamke yule alipomuona alisogea karibu na akasema:
“Nina matatizo. Mume wangu
amenionea. Amenifukuza kwenye nyumba na amenitishia kunipiga. Nakuomba uje
uhukumu haki baina yetu.”
“Ewe mja wa Mungu, kuna joto
jingi hivi sasa, subiri hadi nyakati za jioni joto lipungue ndipo nije
kusawazisha manung’uniko yako.”
“Ikiwa nitachelewa nje kwa muda
mrefu nahofia atakasirika zaidi.” Aliinamisha kichwa chake kwa muda na kisha
akakiinua akijiambia,
“Hapana, ninaapa kwa Mweyenzi
Mungu haifai kuchelewesha hukumu ya mwenye kudhulumiwa. Na haki yake lazima
ichukuliwe kutoka kwa mwenye kudhulumu. Na uoga wowote ule lazima utolewe
kwenye moyo wa mdhulumiwa, ili aweze kusimama imara mbele ya muonevu na kudai
haki yake.”
“Nieleze nyumba yenu iko wapi?”
“Ni mahali fulani.”
“Twende pamoja.”
Aliandamana naye hadi nyumbani
kwake. Walipofika alisimama mlangoni na kuita kwa sauti kubwa, ‘Ewe Bwana
mwenye nyumba! Amani iwe juu yako’
Bwana mwenye umri wa wastani
alijitokeza na ndie alikuwa mume wake. Hakuweza kumtambua Imam Ali (a.s). Alimuona ni mtu mzima mwenye umri wa karibu
miaka sitini ambaye aliandamana na mkewe na akachukulia kuwa amemleta kama
mtetezi na msuluhishaji lakini alinyamaza kimya.
“Mwanamke huyu, ambaye ni mkeo
ana malalamiko dhidi yako. Anadai kuwa wewe umemuonea na kumfukuza nyumbani.
Pamoja na hayo umetishia kumpiga. Nimekuja kukueleza kuwa umuogope Mwenyezi
Mungu na uwe mpole na mkarimu kwa mke wako.” Imam Ali (a.s) alisema.
“Inakuhusu nini kama
sikumtendea vema mke wangu? Ndio, nimetishia kumpiga, lakini kwa sababu
amekuleta wewe ili kumuombea, basi nitamtupa kwenye moto na kumchoma akiwa
hai.”
Imam Ali (a.s) hakufurahishwa
na ukaidi wa yule kijana. Alichomoa upanga wake huku akisema; “Nakushauri tu
kutenda mema na kukukanya kutokana na matendo mabaya (maovu), lakini wewe
unanijibu kwa namna hii ya wazi kuwa utamchoma mwanamke huyu kwenye moto.
Unadhani hakuna mamlaka katika duniani hii?”
Sauti kubwa ya Ali iliwavuta
wapita njia na punde si punde umati mkubwa wa watu ukakusanyika hapo. Kila
aliyekuja aliinama kwa heshima na kumuamkia yule mzee kwa kusema “Amani iwe juu
yako Ewe Kiongozi wa waumini.”
Wakati yule kijana mfedhuli
alipomgundua aliyekuwa akiongea naye, alitetemeka na kuomba, “Ewe kiongozi wa
waumini, nisamehe. Ninakiri makosa yangu na nakuahidi kwamba kutoka leo
nitamtii mke wangu. ”
Imam Ali (a.s) alimgeukia yule
mke na akamwambia aingie nyumbani kwake, kisha alimkanya kutotenda
yatakayomkasirisha mume wake tena.
MAFUNZO
1. Tujiupushe
na hasira kali, mwislamu unatakiwa kuwa na uwezo wa kuidhibiti hasira yako
2. Wanawake
wawe na utii kwa wame zao
3. Imam Ally
alikuwa mtetezi wa haki za binadamu
Comments
Post a Comment