MALIKI ASHTAR, KAMANDA WA
MAJESHI YA KIISLAMU
Wakati fulani, Maalik Ashtar
alikuwa akipita katika soko la Kufah akionekana masikini sana. Alikuwa amevaa
nguo nzito (iliyotengenezwa kwa kitambaa cha turbai) na alikuwa ameweka turbai
kichwani kwake badala ya kilemba.
Mmoja wa wafanya biashara
alikuwa amekaa dukani mwake macho yake yalipoangukia kwa Maalik. Alimtazama kwa
twezo na kwa dharau akamtupia kipande cha udongo.
Maalik alimpuuzia na
aliendelea na safari yake. Hata hivyo mtu aliyemtambua Maalik na aliyekuwa
ameshuhudia tukio hilo, alimkanya mfanya biashara:
“Aibu juu yako! Unamjua
uliyemdhalilisha punde tu?”
“Hapana.” Alijibu mfanya
biashara
“Alikuwa ni Maalik Ashtaar,
sahaba wa imam Ali (as).”
Baridi iliingia mwilini mwa
mfanyabiashara alipowaza juu ya uovu alioufanya. Mara moja aliondoka na
kumfuata Maalik ili akaombe msamaha.
Alibaini kwamba Maalik
alikuwa ameingia msikitini ambako alikuwa akisali na akamua kumsubiri. Maalik
alipomaliza kuswali tu yule mfanya biashara alimuangukia miguuni na kuanza
kuibusu, Maalik alimnyanyua na kumuuliza alichokuwa akifanya.
“Ninaomba msamaha kwa dhambi
niliyofanya,” alijibu mfanya biashara. Maalik akaeleza, “Hakuna dhambi juu
yako. (Naapa) kwa Allah, nilikuja msikitini makhsusi kwa ajili ya kukuombea
msamaha.”
Rejea:
Muntahl Aa’maal, Juz. 1, uk.
212; Majumua’h Warraam - Ibn Abi Farraas
Comments
Post a Comment