MTUKUFU MTUME (SAW) NA
NUA’IMAAN
Nua’imaan Ibn Amr Ansaari
alikuwa ni mmoja wa masahaba wa mwanzo wa Mtukufu Mtume (saw) na alikuwa na
maumbile ya uchangamfu na ukarimu.
Imesimuliwa kuwa siku moja
Bedui mmoja aliwasili Madina na akampumzisha ngamia wake nyuma ya Msikiti
(kisha) akaingia ndani ili awe kwenye hadhara ya Mtukufu Mtume (saw).
Baadhi ya masahaba wa Mtume
walimshawishi Nua’imaan kwa kusema “Ikiwa utamuua ngamia huyu, tutagawana nyama
yake miongoni mwetu, na Mtukufu Mtume (saw) atalipa bei yake kwa mmiliki.”
Kwa kufuata ushauri wao
Nua’imaan alimuua mnyama yule. Mmiliki alipotoka nje ya msikiti na kukuta
ngamia wake amekufa alikasirika sana na akaamua kulileta jambo hili mbele ya
Mtukufu Mtume (saw). Nua’imaan wakati huo alikuwa amekwishakimbia.
Mtukufu Mtume (saw) alitoka
nje ya msikiti, akamuona ngamia aliyekufa na kuuliza “Ni nani anayewajibika kwa
kitendo hiki? Wale waliokuwepo walimtuhumu Nua’imaan, hivyo Mtukufu Mtume (saw)
akamtuma mtu kwenda kumleta Nua’imaan mbele yake.
Habari zilivuma kuwa
Nua’imaan alikuwa amejificha katika nyumba ya Dhubaa’h Bint Zubeir ambayo
ilikuwa karibu na msikiti. Alikuwa ameingia kwenye shimo kisha akajifunika na
majani mabichi. Mtukufu Mtume (saw) alielezwa juu ya maficho ya Nua’imaan na
yeye na masahaba zake wakaelekea kwenye nyumba ya Dhubaa’h walipofika hapo,
mjumbe aliomuonyesha Mtume (saw) maficho ya Nua’imaan ambaye Mtume (saw)
alimuamuru (mjumbe) alifungue shimo. Baada ya kufanyika hilo, Nua’imaan
aliibuka huku mashavu na kipaji chake cha uso vikiwa vimefunikwa na majani
mabichi.
Alipomuona, Mtukufu Mtume
(saw) alimuuliza “Ewe Nua’imaan! Ni nini hiki ulichokifanya?
Aljibu, “Ewe Mtume wa Allah
(Naapa) kwa Allah! hao watu waliokuleta kwenye maficho yangu, ndio hao hao
walionishawishi nimuue ngamia!”
Mtukufu Mtume (saw)
alitabasamu na kufuta majani kutoka kwenye mashavu na kipaji cha uso cha
Nua’imaan kwa mikono yake mitakatifu. Kisha akalipa gharama ya ngamia kwa yule
Bedui kwa niaba ya Nua’imaan.
Hapa tunajifunza kuwa:
1. Tuache
unafiki (tuwe wakweli)
2. Tuache
kudanganyana (kupotoshana)
3. Tuache
watu wajifunze ukweli na pia tuwaache waifuate haki
Comments
Post a Comment