MWENENDO WA IMAM SAJJAD (AS)
Wakati fulani, mwislamu
mwenye kuwachukia Ahlulbayt wa Mtume (s.a.w.w) alimuendea Imam Sajjad (as) na
akaanza kumkashifu na kumtukana. Imam (as) hakutamka neno lolote kumjibu
lakini, baada ya yule mtu kuondoka kwenye mkusanyiko ule, aliwageukia watu
waliokuwepo na kusema:
“Mmesikia aliyosema mtu
huyu, sasa ninataka muambatane na mimi mkasikie kile nitakachosema kujibu
kashfa na matusi yake”
Masahaba wake wakakubali,
“kwa hakika tutaambatana nawe, kwa kusema kweli tulitaraji kuwa ungemjibu
wakati ule ule”
Imam (as) aliondoka kuelekea
kwenye nyumba ya mtu huyo na alisikika akisoma aya ya Qur’ani ifuatayo:
“Na ambao wanazuia hasira
(zao) na wanasamehe (makosa ya) watu; kwani Allah anawapenda wale wafanyao wema
(kwa wengine) (Quran 3: 134)
Msimuliaji anasema:
“Tuliposikia kisomo cha aya hii, tulijua kwamba Imam (as) alikusudia kuonyesha
wema kwa mtu ambaye punde tu alikuwa amemtukana”
Alipofika kwenye nyumba ya
mtu huyo, Imam (as) alimuita na akamjulisha kuwasili kwake. Alipomuona Imam,
yule mtu akajua kuwa amekuja kujibu kashfa zake.
Lakini, mara tu Imam (as)
alipomuona yule mtu, alisema, “Ewe ndugu (yangu)! Ulikuja kwangu na kusema vitu
vya kutisha na visivyopendeza.
Ikiwa uliyoyasema juu yangu
ni ya kweli, (basi) ninaomba msamaha kwa Allah, lakini ikiwa sio, basi
ninamuomba Allah ‘Azza wa Jallah akusamehe.” Yule mtu alishtushwa kusikia
maneno haya na akatubu. Alimbusu Imam (as) baina ya macho na akaomba msamaha,
akisema:
“Matusi yangu na kashfa
hayakuwa na msingi na hayawezi yakahusishwa na tabia yako. Kwa kweli matusi
yale yananistahili mimi zaidi kuliko wewe.”
MAFUNZO KUTOKANA NA KISA
HIKI:
1. Matusi
dhidi ya Mashia na viongozi wake hayakuanza leo
2. Wako
watu wanadai kuwa ni waislamu lakini hawana adabu kwa Mtume wala Ahlulbayt
wake. Watu wa aina hii ni waovu
3. Wafuasi
wa Ahlulbayt wanatakiwa wawe na Subira kama walivyokuwa maimamu watukufu na
wawapuuze wale wanaowasingizia kwa kila aina ya uovu.
4. Waliojijengea
tabia ya kukosa adabu na ubabe dhidi ya waislamu wenzao, hawajachelea, muda wao
wa kutubu ni huu na watubu sasa kabla hawajaingizwa makaburini.
Comments
Post a Comment