FAMILIA YA YASIR
Katika kipindi cha kwanza cha Uislamu, familia ndogo ya watu wanne na iliyokuwa inakandamizwa, ilisilimu. Kila mmoja wao alionyesha kiwango cha juu cha ustahamilivu katika kukabiliana na mateso ya kikatili ya washirikina. Watu hawa wanne walikuwa ni Yasir, mkewe Sumaiyah na waoto wao wawili Ammar na Abdullah.
Yasir alisimama imara katika dini yake akisumbuliwa na kashfa za maadui, hadi hatimaye alipouawa shahidi. Mkewe Sumaiyah licha ya umri mkubwa, kwa ukakamavu alistahamili mateso ya maadui hadi hatimaye Abu Jahl alipompatia jeraha lake la mwisho.
Hivyo Sumaiyah alikufa shahidi kutokana na kipigo katika Tumbo Lake.
Hivyo Sumaiyah alikufa shahidi kutokana na kipigo katika Tumbo Lake.
Abu Jahl, mbali na kumtesa Sumaiyah mwili wake, pia alikuwa akimtesa kisaikolojia wakati (Sumaiyah) alipokuwa mzee na dhaifu. Alikuwa akimuudhi kwa kusema: “Umefuata dini ya Muhammad sio kwa ajili ya Mungu bali kwa sababu umempenda Muhammad na umetekwa na sura yake nzuri.”
Mtoto wa Yasir, Abdullah pia alipewa mateso makubwa lakini yeye pia alibakia imara. Mtoto mwingine Ammar, alikuwa akipelekwa katika jangwa linalounguza, akivuliwa nguo na kuvishwa koti la chuma la moto katika mwili wake uliounguza nusu na kulazimishwa kulala katika mchanga wa moto, na chembe chembe zake zilikuwa kama vipande vya chuma kutoka katika tanuri la mhunzi. Mataokeo yake vyuma vya koti la chuma vilikuwa vikipenya kwenye mwili wa Ammar na walikuwa wakimuambia “mkane Muhammad (saw) na uwaabudu Lat na Uzza,” lakini Ammar kamwe hakusalimu amri kutokana na mateso yao.
Chuma kilichoungua kiliacha alama katika mwili wake kiasi kwamba Mtukufu Mtume (saw) alipomuona Ammar alikuwa anaonekana kufanana na mtu mwenye ukoma.
Alama kama za ugonjwa huo zilionekana usoni, mikononi na katika mwili wa Ammar (na) zilifanya aonekane kama mkoma.
Alama kama za ugonjwa huo zilionekana usoni, mikononi na katika mwili wa Ammar (na) zilifanya aonekane kama mkoma.
Mtukufu Mtume (saw) alikuwa akisema hivi juu ya familia ya Yasir: “Enyi familia ya Yasir! Kuweni na subira na bakieni imara, kwani bila shaka peponi ndio makazi yenu”1
Rejea:
1. Hikaayaat -ha- e- Shanidan, Juz.5, uk. 25,
1. Tafsir al-Manaar, Juz. 2, uk . 376
1. Tafsir al-Manaar, Juz. 2, uk . 376
Comments
Post a Comment