HADITHI YA NDEGE:
Imepokewa na Anas Ibn Malik, Anasema: Nilikuwa Nikimtumikia Mtume (s), Mara Mtume (s) Akaletewa Ndege Aliyechomwa-akasema "ewe Mola Wangu Niletee Kiumbe Umpendaye Zaidi Ili Ale Pamoja Nami Ndege Huyu", Nikasema "mola Wangu Mjaalie Awe Katika Maanswari(wenzangu)".
Mara Akaja Aliy (ra), Nikamwambia Mtume (s) Ana Shughuli, Aliondoka Kisha Akarejea Tena, Nikamwambia Mtume (s) Ana Shughuli, Akaondoka Kisha Akarejea Tena, Mtume (s) Akamwambia Ingia, Alipoingia,Mtume (s) Akamuuliza Kipi Kilichokufanya Usije Kwangu? Akasema "Hii Ni Mara Ya Tatu Nakuja Lakini Anas Ananirudisha Kwa Madai Una Shughuli",
Mtume (s) Akaniuliza Ni Kipi Kilichokufanya Ufanye Hivyo? Nikamjibu" Ya Rasulullah! Nilisikia Du'a Yako Kwa Hiyo Nikapenda Aje Mtu Katika Ahali Zangu" Mtume (s) Akasema : Hakika Hakika Mtu Huwapenda Ahali Zake.
-REJEA
Al-mustadrak Ala Swahiyhayn Juzuu.3,uk.130 Hadi 131. Sunan Tirmidhiy Juz.5 Uk 636-637.
Comments
Post a Comment