IMAM ALI (AS) APAMBANA NA
AMR
Amr Ibn Abd Wuud alikuwa ni
mpiganaji ambaye, katika vita alikuwa ni sawa na askari 1000. Katika vita vya
Ahzaab, aliwapa changamoto askari wa Kiislamu kupigana naye, lakini hakuna hata
aliyekuwa na ujasiri wa kusimama mbele yake hadi Imam Ali (as) alipokwenda
mbele ya Mtukufu Mtume (saw) na kuomba ruhusa ya kupigana naye.
Mtukufu Mtume alimuambia Ali
(as): “Tambua kuwa huyu ni Amr Ibn Abd Wuud!” Imam Ali (as) kwa unyenyekevu
alisema “(Na) mimi ni Ali Ibn Abi Talib,” na kisha akaenda katika uwanja wa vita
na kusimama mbele ya Amr.
Baada ya mapambano makali,
Imam (as) hatimaye alimuangusha chini na akakaa juu ya kifua chake. Walipoona
hivi, jeshi zima la Waislamu lilimuomba Mtukufu Mtume (saw): “Ewe Mjumbe wa
Allah, muamuru Ali (as) amuue Amr mara moja!”
“Muacheni kwani anayajua
matendo yake vizuri zaidi kuliko mwingine yeyote,” alijibu Mtukufu Mtume (saw).
Ali (as) alipokuwa amekikata
kichwa cha Amr, alikileta kwa Mtukufu Mtume (saw) ambaye alimuuliza “Ewe Ali!
Ni nini kilichokufanya usite kabla ya kumuua Amr?
Akasema, “Ewe Mjumbe wa
Allah! Nilipokuwa nimemwangusha chini, alinikashifu matokeo yake nikapatwa na
hasira. Nilihofia kuwa kama ningemuua katika hali ile ya hasira, ingekuwa
(nimemuua) kwa ajili ya kijifariji na kuiridhisha roho yangu.
Hivyo niliondoka juu yake
mpaka hasira yangu ilipokwisha na nikarudi kukitenganisha kichwa chake kutoka
katika mwili kwa ajili ya furaha ya Allah na kwa ajili ya kumtii Yeye.”
Ilikuwa ni kwa sababu ya
unyofu na pigo lenye thamani kwa upande wa Imam Ali (as) kwamba Mtukufu Mtume (saw)
alisema: “Dhoruba la upanga wa Ali katika siku ya vita vya Khandaaq ni bora
kuliko ibada ya wanadamu wote na majini.”
REJEA:
Pand –e- Tarikh, Juz 5, uk. 199; Anwaar al-
Nu’maaniyah;
Comments
Post a Comment