IMAM AU KHALIFA WA KWANZA WA WAISLAMU, ALIYETEULIWA NA MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W)
Naye ni Ali bin Abi Talib (a.s.), na mama yake ni Fatima binti Asad, Ibnu Ami Rasulillahi: na mume wa binti wake Mtume (s.a.w.w.). Ndiye Khalifa juu ya watu baada yake, naye ni Amirul Muuminiin (Mkuu wa walioamini), mzazi wa Maimamu wote (juu yao Amani na Rehema).
Kazaliwa bwana huyu Kaabani (ndani ya Kaaba [3] Tukufu) Maka, siku ya Ijumaa, usiku wa mwezi kumi na tatu, mfungo kumi, baada ya kupita miaka thelathini toka kuzaliwa Mtume (s.a.w.w.).
Na akawa shahidi (akauawa kwa ajili ya dini) usiku wa Ijumaa ndani ya msikiti wa Kufa mihirabuni [4] kwa kupigwa upanga na Abdur-Rahman bin Muljimu (Mungu amuweke pabaya), usiku wa mwezi kumi na tisa, mwezi wa Ramadhani Mtukufu; akafa siku ya tatu toka kupigwa. Na umri wake mtukufu ni miaka sitini na tatu.
Akasimamia matengenezo ya mazishi yake Imam Hassan na Hussein (a.s.), na akazikwa katika Najaf (Iraq) alipokuwepo sasa.
Akasimamia matengenezo ya mazishi yake Imam Hassan na Hussein (a.s.), na akazikwa katika Najaf (Iraq) alipokuwepo sasa.
Bwana huyu mwema asiye na makuu na fadhila (ubora) zisizo hesabika. Amekuwa ni mtu wa kwanza kuamini; wala hakusujudia sanamu hata kidogo, na hakupata kushindwa vita vyovyote alivyo viongoza, wala hakuwahi kukimbia kunako mashambulizi yoyote ya maadui.
Na katika jumla ya fadhila zake, Mtume (s.a.w.w.) kasema:-"AQDHAKUM ALIYUN", Kadhi mwenye kuamua vizuri kuliko wote ni Ali (a.s.)-
Na katika uwingi wa elimu yake, Mtume (s.a.w.w.) kasema, "ANAA MADINATUL -ILMU WA ALIYUN- BAABUHA", Mimi ni Jiji la Elimu na Ali (a.s.) ni lango lake.
Na katika uwingi wa elimu yake, Mtume (s.a.w.w.) kasema, "ANAA MADINATUL -ILMU WA ALIYUN- BAABUHA", Mimi ni Jiji la Elimu na Ali (a.s.) ni lango lake.
Basi inatuonyesha kwamba atakaye elimu ya Mtume (s.a.w.w.) ni lazima apitie mlangoni na ufunguliwe, na kama hakufunguliwa basi hana elimu, na kufunguliwa kwake ni kufuata mafunzo yake na mwenendo wake Imam Ali (a.s.).
Na katika kulazimiana na Haki, basi Mtume (s.a.w.w.) kasema, "ALIYUN MAAL-HAKKI WAL-HAKKU MAA ALIY", Ali yu pamoja na Haki na Haki ipo pamoja na Ali.
Sina shaka wasemi wamesema kama mtambuzi, tambua wewe mwenyewe.

Na alikuwa mwadilifu kwa raia wake, mgawa kwa usawa,
mchamungu katika mshuko wa ulimwengu.
mchamungu katika mshuko wa ulimwengu.
Alikuwa akienda katika idara ya mali (Hazina) na hutazama dhahabu na fedha na husema: "Ee ung'avu wake! Ee uweupe wake! Umkhadaae mwingine, siyo mimi". Kisha hugawa kwa watu.
Alikuwa anawahurumia maskini, hukaanao mafakiri; huwatekelezea wenye shida, na husema ukweli, na huhukumu kwa uadilifu.
Na kwa ujumla, yeye alikuwa kama Mtume katika kila sifa mpaka akamjaalia Mungu Mtukufu, katika aya ya Qur'an, kuwa yeye ni "Nafsi ya Mtume”
KABURI TUKUFU LA IMAM ALI HUKO NAJAF.
Comments
Post a Comment