MALIPO YA MASHAIRI
Siku moja ya Nawruz, Mansur Dawaaniqi, Khalifa kutoka ukoo wa Bani Abbasi aliyechukua ukhalifa baada ya kaka yake Abu al-Abbas Saffaah, alimuamuru Imam Musa Kadhim (as) kuhudhuria katika Eid ya Nawruz, ilifanywa hivi ili watu waje na kumsalimia na kumpa zawadi ambazo alipaswa kuzikubali.

Imam (as) alimuambia Mansur, “Nawruz ni Eid ya kimila ya Wairan hakuna kilichotajwa juu yake katika Uislam”
Juu ya hili Mansur alijibu “kitendo hiki kina hamasa za kisiasa na inakusudiwa kuwafurahisha askari wangu. Ninakuweka chini ya Mola mkuu kuwa ukubali ombi langu na uhudhurie katika mkusanyiko huo.” Imam (as) alikubali na akawasili katika hadhara ya Majenerari wa jeshi, Mamwinyi na watu wa kawaida walipita mbele yake wakamsalimia na kumpa zawadi zao.
Wakati huo huo Mansur alikuwa amemuamuru mmoja wa watumwa wake akae karibu na Imam akitunza kumbukumbu ya fedha na zawadi zinazowasilishwa kwake.
Mtu wa mwisho kuja kumuona Imam (as) alikuwa ni mzee aliyemuambia: “Ewe mtoto wa Mjumbe wa Allah! Mimi ni mtu masikini na sina fedha za kukununulia zawadi, lakini zawadi yangu kwa leo ni aya tatu za shairi la maombolezo, ambazo babu yangu amezitunga kwa ajili ya babu yako, Husein Ibn Ali (as).” Baada ya kusema hayo akasoma aya hizo.
Imam (as) alishukuru kwa kusema; “Nimeikubali zawadi yako” kisha akamsomea dua mtu huyo. Kisha akamgeukua mtumwa na kumuagiza “Nenda kwa Mansur mjulishe juu ya zawadi hizi na muulize zifanyweje.” Mtumwa alifanya kama alivyoagizwa na aliporudi, alimuambia Imam (as): “Khalifa amesema: “Amekupa wewe (Imam Musa Kadhim) kama zawadi, zitumie utakavyo.”
Imam (as) alimuambia yule mzee: “Chukua utajiri huu na zawadi hizi, kwani ninakupatia vyote hivi kama zawadi.”
Rejea:
Muntahal Aamal, Juz 2 uk.187
Muntahal Aamal, Juz 2 uk.187
MAZINGATIO
1. Imam Mussa Kadhim alikuwa khalifa (wa Mtume) halali wa saba, wa kwanza akiwa ni imam Ally bin Abi Talib
2. Mansur alikuwa khalifa wa bandia ambaye ni zao la kugombea madaraka kuliko fanywa na Abubakar na wenziwe kule Saqifah
3. Kumlilia imam Hussein ni ibada ambayo ilianzishwa na Mtume na kuendelezwa na Maimamu (makhalifa) wa kiislamu wote.
4. AhlulSunnah ni wa kwanza kufuata mila za wairan halafu wanawasingizia Mashia.

Comments
Post a Comment