MUUZA DUKA MPUMBAVU
Bwana mmoja mrefu mwenye misuli
alikuwa akipita kwenye soko la mji wa Kufa, hatua zake zikuwa imara na za
uhakika. Alikuwa na umbo zuri na uso uliobabuka na jua; mapambano kwenye uwanja
wa vita yameacha alama kwenye mwili wake na pembeni ya moja ya jicho lake
palikuwa na mpasuko.
Mchuuzi mmoja, kwa
kuwafurahisha marafiki zake, alimwagia taka mwilini mwake. Yule bwana
aliendelea kutembea vile vile bila ya kubadili mwendo wala kumuangalia yule
muuza duka. Alipokuwa amekwenda, mmoja wa marafiki wa yule mchuuzi alimuuliza:
“Je huyu bwana uliyemfanyia
ufedhuli hivi punde unamjua ni nani?” akajibu, “La simtambui, alikuwa ni mpita
njia tu kama wengine wanaopita hapa kila siku. Lakini hebu niambie, ni nani mtu
yule?”
“Ajabu! Hamkumjua? Alikuwa ni
Malik Ashtar, amiri jeshi mkuu maarufu wa Ali.”
“Ni ajabu kweli! Ashtar huyu
huyu ambaye ujasiri wake hugeuza moyo wa simba kuwa maji na ambaye kutajwa kwa
jina lake hufanya maadui zake watetemeke kwa hofu?”
“Ndio, yule alikuwa ni Malik
Ashtar mwenyewe!”
“Ole wangu! nimefanya nini?
Sasa atatoa amri ya kuniadhibu vikali. Ni lazima nimkimbilie sasa hivi
nikamtake radhi na kumuomba msamaha kwa adabu yangu mbaya”
Alimkimbilia Malik. Akamuona
akigeuka kuelekea msikitini, alimfuata hadi msikitini na kumkuta tayari ameanza
kuswali. Alingojea hadi alipomaliza kuswali.
Kwa unyenyekevu kabisa
alijitambulisha na akamuambia; “Mimi ndiye yule bwana ambaye ametenda kitendo
cha ujinga na kutokuwa na adabu mbele yako”
Malik akamwambia; “Wallahi
sikuja msikitini bali ni kwa ajili yako; kwa sababu nilijua kuwa wewe ni mtu
jahili na mpotofu na unawapa watu taabu bila ya sababu. Nilikuonea huruma na
nimekuja kukuombea na kumuomba Mwenyezi Mungu akuongoze kwenye njia sahihi.
Hapana, kamwe sikuwa na
madhumuni kama hayo yaliyokufanya ukawa muoga. Sikukusudia kukuadhibu wala
kulipiza kisasi kwa uchafu ulionifanyia.
Comments
Post a Comment