NABII NUHU (AS)
Nabii Nuh (as) aliishi maisha marefu na magumu ambayo yalitokana na kutumia muda mwingi miongoni mwa waabudu masanamu wagumu, akijaribu kuwaondolea imani zao za uongo. Hata hivyo licha ya hilo alistahamili na kuonyesha uimara bila kujali mateso na matatizo yao.
Wakati fulani watu walikuwa wakimpiga kiasi cha kupoteza fahamu kwa siku tatu nzima huku damu zikiendelea kutoka kwenye masikio yake. walikuwa wakimkamata na kumtupa ndani ya nyumba, lakini akirudiwa na fahamu alikuwa akiomba dua:
“Ewe Mola! Waongoze watu wangu kwani hawaelewi!”
“Ewe Mola! Waongoze watu wangu kwani hawaelewi!”
Kwa takribani miaka 950 alikuwa akiwaita watu kwa Allah, lakini watu ndio kwanza walikuwa wanazidisha uasi wao na ukaidi. Walikuwa wakiwaleta watoto wao kwa Nuh (as) wakiwaonyesha na kusema:
“Enyi watoto! Ikiwa mtatokea kuishi baada yetu, kuweni waangalifu kutomfuata mtu yeyote kichaa!” Kisha walikuwa wakimuambia, “Ewe Nuh! usipoacha hutuba zako, utapigwa mawe mpaka ufe. Hawa watu wanaokufuata, ni duni na dhalili, ambao wamesikia mazungumzo yako na kuukubali wito wako bila kutafakari na kuchunguza.”
Nuh (as) alipokuwa anaongea nao, walikuwa wakitia vidole vyao masikioni na kuvuta nguo zao kichwani ili wasisikie maneno yake wala kumuona uso wake. Mambo yalifikia hali isiyovumilika kiasi kwamba Nuh (as) alikosa cha kufanya isipokuwa kuomba msaada wa Allah na hivyo aliomba dua: “Ewe Allah! Nimezidiwa nguvu, nisaidie na niepushe nao.” 1
Rejea:
1. Taarikh –e- Anbiyaa, uk. 48-52
1. Taarikh –e- Anbiyaa, uk. 48-52
Comments
Post a Comment