NABII YUSUF (AS) NA NDUGUZE
Miaka kadhaa baada ya tukio la nduguze Yusuf (as) kumchukuwa kwa udanganyifu nje ya mji. Kumpiga na kumtupa kisimani na hivyo kumlazimisha baba yao kulia mfulululizo na kusonononeka kwa hasara yake, wale ndugu walisikia kuwa Yusuf amekuwa waziri wa Misri. Wao na baba yao walienda kuonana naye.
Sentensi ya kwanza kabisa ambayo Yusuf aliitamka alipowaona, ilikuwa:
Sentensi ya kwanza kabisa ambayo Yusuf aliitamka alipowaona, ilikuwa:
“Na kwa hakika alikuwa mwema kwangu aliponitoa gerezani…”1
Inavyooneka ni kwa sababu ya tabia njema kwamba Yusuf aliepuka kutaja matatizo aliyoyapata; kwanza kutupwa kisimani, kisha kufanywa kwake mtumwa na kisha matukio yasiyofurahisha, aliyokumbana nayo kutokana na matendo ya nduguze. Hakutaka kufufua kumbukumbu hizo chungu, ambazo zingewasababishia fedheha na mfadhaiko.
Kisha aliongeza, “Ni shetani aliyewashawishi ndugu zangu kunifanyia yale matendo yasiyofaa, kunitupa kisimani na kunitenganisha na baba yangu; hata hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu alinifanyia wema kwani aliyafanya matendo hayo kuwa ni njia ya kuipatia familia yetu utukufu na heshima!”
Kuyahusisha matendo ya kidhalimu na nduguze na shetani na kumuona yeye (shetani) kama mhusika mkuu wa uhalifu wa nduguze, ulikuwa ni mfano mwingine wa ukarimu na moyo wa kusamehe wa Yusuf. Hivyo aliwakinga dhidi ya mfadhaiko na akawaacha na fursa ya kuomba msamaha kwa matendo yao.
Alisema:
“Hakutakuwa lawama dhidi yenu (kuanzia) siku hii (Quran 12:92)
Alisema:
“Hakutakuwa lawama dhidi yenu (kuanzia) siku hii (Quran 12:92)
Kaeni kwa amani juu yangu, kwani nimewasamehe na nimeyasahau yote yaliyotokea, na kwa niaba ya Mwenyezi Mungu pia, ninaweza kuwapeni habari njema na tafuteni kutoka kwake ili Allah awasamehe na Yeye ni Mwenye rehema kuliko wenye rehema wote.2
“Kwa hakika yule ajichungaye (dhidi ya maovu) na akawa na subira (hulipwa) kwani kwa hakika Allah huwa hapotezi ujira wa wafanyao wema.” (Qur’an 12:90)
Somo ambalo nabii Yusuf (as) alimfundisha kila mmoja ni lile la kuonyesha wema na ukarimu kama majibu ya tabia mbaya, na tunataraji sisi pia tunaweza kufanya hivyo kwa ndugu zetu katika Iman, Inshaallah!
1. Qur’ani Tukufu Suratul Yusuf 12:100
2. Qur’ani Suratul Yusuf 12:92
2. Qur’ani Suratul Yusuf 12:92
Mazingatio:
1. Kumlilia mtu anayekumbwa na msiba ni sunnah ya nabii Yaqub (a.s). yeye alimlilia Yusuf mpaka akapofoka macho
2. Watu waovu wapo tu, haijalishi wanataokana na kabila gani
3. Uislamu umehimiza sana usamehevu na kupiga vita tabia za kujichukulia sheria mikononi
1. Kumlilia mtu anayekumbwa na msiba ni sunnah ya nabii Yaqub (a.s). yeye alimlilia Yusuf mpaka akapofoka macho
2. Watu waovu wapo tu, haijalishi wanataokana na kabila gani
3. Uislamu umehimiza sana usamehevu na kupiga vita tabia za kujichukulia sheria mikononi
Comments
Post a Comment