OMBI LA NABII MUSA (AS)
Nabii Musa alipata kumuomba
Allah:
“Ewe Mola! Ni utashi wangu
kumuona kiumbe wako aliyejitakasa kwa ajili ya ibada Yako na ambaye
hajachafuliwa katika utii wake Kwako” Aliambiwa: “Ewe Musa! Nenda katika fukwe
za bahari fulani ili nikuonyeshe unachotaka kukiona”
Nabii Musa alikwenda mpaka
akafika karibu na bahari. Alipotazama pembeni, aliona kuwa tawi la mti
lililokuwa limeinamia juu ya maji, alikuwa amekaa ndege, akiwa amezama katika
kumdhikiri Allah.
Musa alipomuuliza ndege
(habari zake), ndege alisema: “Tangu Allah aliponiumba, nimekuwa katika tawi
hili, nikimuabudu Yeye na dhikiri. Kwa kila dhikiri yangu moja hutokea dhikiri
1000 nyingine, na furaha ninayoipata kutokana na dhikiri ya Allah hunipatia
virutubisho.”
“Je unatamani kitu chochote
katika ulimwengu huu?”Aliuliza Musa (as). “Ndio. Ninatamani sana kuonja tone
moja la maji kutoka kwenye bahari hii.” alijibu ndege. Musa (as) akasema kwa
mshangao “Lakini hakuna umbali mkubwa kati ya mdomo wako na maji! Kwa nini hutumbukizi
mdomo wako ndani (ya maji) na kunywa?”
Ndege akajibu, “kutokana na
hofu kwamba isije ikawa raha inayotokana na maji ikanifanya nisahau raha ya
kumdhukuru Mola wangu.” Aliposikia hivi, Nabii Musa (as) alishika kichwa chake
kwa mshangao mkubwa.
REJEA:
Khazinah al- Jawaahir, uk.
318
Comments
Post a Comment