UNYOFU (UTAKASAJI WA NAFSI)
Allah Mwenye hikma, amesema:
“Hivyo muabuduni Allah (peke yake) mkiwa
waaminifu Kwake katika dini.” (Quran 39:2)
Imam Ali (as) alisema:
“Fanya matendo yako kwa unyofu, kwani (ukifanya hivyo) hata kidogo kitakutosha.1
Maelezo mafupi:
Unyofu ni ufunguo wa
kukubaliwa amali zote. Mtu ambaye amali zake zimekubaliwa na Allah hata ziwe
ndogo kiasi gani, ni mtu mnyofu na mtu ambaye amali zake zimekataliwa na Allah,
licha ya wingi wake, sio miongoni mwa watu wanyofu.
Mtu mnyofu hujitahidi
kuitakasa roho yake kutokana na maovu na hujibadilisha kufanya amali njema na
kudumisha (unyofu wa) nia ili Allah azikubali amali zake.
Kiwango cha nia, maarifa na
matendo yanahusiana na utakaso wa kiroho na usafi (wake), na kama mtu mnyofu
angezingatia kikamilifu nafsi yake ya ndani, angeitambua dhana halisi ya upweke
wa Allah. Kiwango cha chini kabisa cha unyofu ni wakati mtu anapofanya jitihadi
kwa kadiri ya uwezo wake wote, akiwa hatarajii malipo kwa matendo yake wala hayapi
umuhimu wowote.
Rejea:
1. Jaame’
al Saadaat Juz. 2, uk. 404 2.
2. Tadhkirah
al Haqaaiq, uk 73
Comments
Post a Comment