USTAHAMILIVU (SUBIRA)
Allah mwenye Hekma Anasema:
“Kisha simama imara (Ewe Mtume Muhammad) katika njia iliyonyooka kama ulivyoamrishwa (na Mola wako) pamoja na wale waliomgeukia Allah pamoja nawe. (Quran 11:112)
“Kisha simama imara (Ewe Mtume Muhammad) katika njia iliyonyooka kama ulivyoamrishwa (na Mola wako) pamoja na wale waliomgeukia Allah pamoja nawe. (Quran 11:112)
Imam Sadiq (as) anasema:
“Muumini yeyote anayepatwa na balaa na kisha akafanya subira, atalipwa thawabu sawa na mashahidi 1000.”1
“Muumini yeyote anayepatwa na balaa na kisha akafanya subira, atalipwa thawabu sawa na mashahidi 1000.”1
Maelezo mafupi:
Kuvumilia na kustahamili kunaweza kupunguza ukali wa mabalaa na misiba. Mtu mwenye imani huwa haonyeshi ukosefu wa subira anapo patwa na mitihani, ili imani yake isiathirike.
Kuvumilia na kustahamili kunaweza kupunguza ukali wa mabalaa na misiba. Mtu mwenye imani huwa haonyeshi ukosefu wa subira anapo patwa na mitihani, ili imani yake isiathirike.
Imesemwa: “Muumini ni imara zaidi kuliko mlima. Hii ni kwa sababu (yeye) ni imara mbele ya maadui na kuonyesha ukakamavu wakati wa mabalaa kiasi kwamba huzuni huwa haipati nafasi katika moyo wa muumini mkamilifu.
Maisha, pamoja na matatizo yake mengi, hayataleta tatizo kwa wale wenye mioyo migumu. Ni wale tu ambao hawana unyofu katika ustahamilivu wao ndio huvunjika moyo wanapopatwa na msiba hata mdogo kabisa. Na ijulikane kama dini ya Allah imetufikia leo hii, ni kwa sababu ya ustahamilivu wa Mtukufu Mtume (saw) na subira ya Imam Ali (as).
1. Mtume alipigwa na kuteswa lakini hakuacha kazi ya kulingania Uislamu
2. Ndiyo hivyo hivyo imam Ally alikuwa bega kwa bega na Mtume na hakurudi nyuma hata siku moja
2. Ndiyo hivyo hivyo imam Ally alikuwa bega kwa bega na Mtume na hakurudi nyuma hata siku moja
3. Baada ya Mtume kufariki, baadhi ya waislamu wakanyakua madaraka kwa nguvu na yeye akawekwa pembeni. Kwa upole na uvumilivu alivumilia hata pale alipofungwa kamba na kupelekwa kwa Abubakar kumbai kwa lazima bado alivumilia, hakupigana japokuwa nguvu alikuwa nazo.
4. Mtume alipofariki, imam Ally na familia yake kwa ujumla walinyimwa mirathi na Abubakar, mali za Mtume akajirithisha mwenyewe. Mbaya zaidi hata mali zao wenyewe walinyang’anywa ili kuwafanya ombaomba na kuwalazimisha utii. Bado alivumilia.
5. Katika hali hii, endapo kama imam Ally angechukua panga na kupambana bila shaka Uislamu ulikuwa hatarini kwa sababu maadui wa Uislamu walikuwa wamejipanga waone udhaifu tu wawavamie na kuufuta Uisilamu.
Rejea:
1. Jaamae’ al –Saadaat, Juz.3, uk. 404
1. Jaamae’ al –Saadaat, Juz.3, uk. 404
Comments
Post a Comment