UZEE NA KUSTAAFU
Mzee mmoja alifanya kazi maisha
yake yote; lakini hakuweza kujiwekea akiba ya siku za uzeeni. Na nyakati zake
za mwisho alikuja kuwa kipofu pia.
Uzee, umaskini na upofu
viliungana mkono, hivyo basi alikuwa hana njia nyingine isipokuwa kuomba.
Alikuwa akisimama pembezoni mwa njia kwa ajili ya kuomba. Watu walikuwa
wakimwonea huruma na kumpa sadaka ambayo alitumia kwa chakula chake kila siku
na hivyo basi aliendelea na maisha yake ya huzuni.
Siku moja imam Ali, Kiongozi wa
Waumini alipitia kwenye njia hiyo na kumwona muombaji huyo katika hali hiyo, na
kutokana na kujali maslahi ya wengine Ali aliuliza kuhusu huyo mzee. Alikuwa
anataka kujua sababu ambazo zilimfanya awe katika hali hiyo. Alikuwa hana mtoto
wa kumsaidia? Ama hakuna njia nyingine ya yeye kuishi maisha ya kuheshimika
katika uzee wake?”
Watu ambao walimjua mzee huyo
walisogea mbele na kumjulisha Ali (a.s.) kuwa alikuwa mkristo na alifanya kazi
kwa bidii kwa muda mrefu alipokuwa na macho yake, na ni kijana mwenye nguvu
zake. Lakini sasa alivyopoteza ujana wake na pia akawa kipofu hakuweza kufanya
kazi yeyote; pia hana chochote alichojiwekea akiba hivyo basi kumlazimu aombe.
Imam Ali (a.s) akasema: “Ajabu!
Alipokuwa na nguvu mlifaidika na kazi za nguvu zake, lakini sasa mumemtelekeza
peke yake?”
Kisa chake hiki kinaonesha kuwa
alifanya kazi alipokuwa na nguvu. Kwa hivyo ni wajibu wa Serikali na Umma
kumsaidia hadi atakapofariki. Nendeni mkampe malipo ya maisha ya uzeeni kutoka
Hazina ya Taifa.
Hivi ndivyo viongozi wa
kiislamu walivyo, humsaidia kila mtu bila kujali dini yake. Ukimwona mtu
anajifanya mwislamu halafu kazi yake kuwafanyia fitina watu, hata kama sio wa
dini yake basi jua wazi kuwa mtu huyo ni mnafiki, kamwe hawezi kuwa mwislamu wa
kweli.
Comments
Post a Comment