WATU WATATU KATIKA PANGO
Mtukufu Mtume (saw)
amesimulia:
“Watu watatu kutoka katika
kabila la Bani Israil walikusanyika na wakaanza safari, walipokuwa njiani,
mawingu yalikusanyika na mvua kubwa ikaanza kunyesha na hivyo wakatafuta
hifadhi katika pango lililokuwa karibu.
Ghafla jiwe kubwa
lilibilingika na kuziba lango la pango, (na hivyo) kuwakwamisha watatu hao
ndani na kuubadili mchana kuwa usiku kwa giza. Walikuwa hawana jingine la
kufanya isipokuwa kumgeukia Allah kwa msaada.
“Tutumie matendo yetu ya
unyofu kama njia ya kupata nusra kutokana na tatizo hili,” alishauri mmoja wao.
Wengine wote walikubaliana na ushauri huo. Mmoja wao alisema “Ewe Mola! Unajua
kuwa nina binamu yangu anayevutia sana kabisa na kwamba nilivutiwa naye na
kumpenda sana, siku moja nilipomkuta akiwa peke yake, nilimchukua na nilitaka
kukidhi matamanio yangu ya kimwili, aliposema: ‘Ewe binamu yangu! Muogope Allah
na usiuharibu ubikra wangu.’
Niliposikia hivi nilivunjilia
mbali matamanio yangu ya kimwili na nikaamua kutofanya kitendo kiovu.
Ewe Mola! Ikiwa kitendo
changu hicho kilitokana na unyofu wa kweli na kwa nia ya kupata radhi Zako tu,
tunusuru kutokana na huzuni na adhabu. Ghafla waliona kwamba lile jiwe
limesogea kidogo, likiruhusu mwanga hafifu kuingia ndani ya pango.
Mtu wa pili alisema: “Ewe
Mola! Unajua kwamba nilikuwa na baba na mama, walikuwa wazee sana kiasi kwamba
miili yao ilikuwa imepinda kutokana na umri uliopindukia, na kwamba nilikuwa
nikiwahudumia kila mara.
Usiku mmoja nikiwa nimewaletea
chakula, nilibaini kwamba wote walikuwa wamelala. Nilikesha usiku kucha karibu
yao, na chakula mkononi, bila kuwaamsha nikihofia kuwasumbua. Ewe Mola! Ikiwa
kitendo changu hiki kilikuwa ni kwa ajili ya kupata radhi na furaha Yako, tufungulie
njia na tupe wokovu.” Alipomaliza kauli yake, kundi lile lilibaini kuwa jiwe
lile lilikuwa limesogea pembeni zaidi.
Mtu watatu aliomba: “Ewe
Mjuzi wa yaliyofichikana na yaliyo dhahiri! Unajua mwenyewe kwamba nilikuwa na
mfanyakazi aliyekuwa akinifanyia kazi. Mkataba wake ulipokuwa umefikia mwisho,
nilimkabidhi ujira wake, lakini hakuridhika na alitaka zaidi na katika hali ya
kutoridhika na kutofurahi, aliondoka.
Nilitumia ujira wake
kununulia mbuzi, na niliwahudumia tofauti, na punde nikawa na kundi la mbuzi.
Baada ya kipindi fulani, yule mfanyakazi alinijia akitaka ujira wake na
nikamuonyesha kundi la mbuzi.
Awali alifikiri
ninamdhihaki, lakini baadaye alipotambua umakini wangu alichukua kundi lote (la
mbuzi) na kuondoka. Ewe Mola! Ikiwa kitendo hiki kilisukumwa na unyofu na
kilikuwa kwa ajili ya kutaka radhi Zako, tuokoe katika mkwamo huu”
Kufikia hapo jiwe lote
liliondoka katika lango la pango na wote watatu wakatoka, wakiwa na furaha na
msisimko, na wakaendelea na safari yao.
Rejea:
1. Katika
kitabu Mahaasim imetajwa kwamba ujira wake ulikuwa ni nusu dirham lakini
alipokuja kuchukua, alipewa mara 18,000 zaidi!
2. Naamunah-e-ma’arif
, Juz.1, uk. 53;
3. Farajun
Ba’d al shiddah, uk 23;
4. mahaasin
e- Barqi, Juz. 2, uk 253
Comments
Post a Comment