WEMA WA IMAM HUSEIN (AS) KWA MPANDA NGAMIA
Imam Jaafar Sadiq (as) alisema: “Mwanaume mmoja alikuwa akimvuta mwanamke alipokuwa (mwanamke) amejishughulisha katika kutufu Kaaba. Mwanamke huyu alikuwa akinyanyua mikono yake, mwanaume yule alipoweka mkono wake juu ya mkono wake (mwanamke), wakati huo Allah aligundisha mkono wake katika mkono wa mwanamke.
Watu walimiminika (kwenda) kushuhudia tukio hili la ajabu kwa wingi mkubwa kiasi kwamba utembeaji ulikwama. Mtu mmoja alitumwa kwa Amiri wa Makka kumjulisha juu ya tukio hili.
Alikusanya wanazuoni wote na kwa ujumla wakajaribu kutafuta suluhisho la tatizo hili. Watu wengi pia wa kawaida walikusanyika wakitaka kujua hukumu itakayotolewa kwa uhalifu huu. Wote wakiwa wamesimama (huku) wametatizika, hatimaye Amiri alisema: “Je kuna mtu yeyote hapa kutoka katika familia ya Mtukufu Mtume (saw)?”
Wale waliokuwepo wakasema, “Ndio! Husein Ibn Ali (as) yupo hapa” Usiku ule Amiri aliamuru Imam (as) akaletwe mbele yake.
Alitaka kujua hukumu ya tukio hili kutoka kwa Imam (as)
Kwanza, Imam (as) aligeukia Ka’aba na kunyoosha mikono yake alisimama katika hali hii kwa muda kisha akaomba dua.
Kisha alimfuata mwanaume yule akautenganisha mkono wake kutoka katika mkono wa yule mwanamke kwa nguvu ya Uimam wake. Yule Amiri alimuuliza Imam (as): “Ewe Husein (as) nimuadhibu?” “Hapana,” alijibu Imam (as).

mwandishi anasema huu ulikuwa ni wema ambao Imam (as) aliuonyesha kwa mpanda ngamia lakini ni mtu huyu huyu aliyelipa kitendo hiki cha wema kwa kukata mikono ya Imam ili akwapue mkanda wake, katika giza la usiku wa 11 Muharram 61H.A.
REJEA:
Raahinama –e- Sa’adat, Juzu ya 1 ukurasa wa 36;
Shajarah-e-Tuba, ukurasa wa 422
Raahinama –e- Sa’adat, Juzu ya 1 ukurasa wa 36;
Shajarah-e-Tuba, ukurasa wa 422
Comments
Post a Comment