WEWE SIO DUNI KULIKO MCHWA

WEWE SIO DUNI KULIKO MCHWA
Amir Taimur Gurgaan, alikuwa ni mtu imara na asiyeyumba katika kila tatizo, kiasi kwamba alikuwa haogopeshwi na tatizo lolote.
Alipoulizwa sababu ya sifa hii, alisema: Wakati fulani nikiwa nimewakimbia maadui zangu na nikitafuta hifadhi katika gofu, nilikuwa nikitafakari juu ya hatma yangu ghafla macho yangu yalipomuangukia mchwa mdogo na dhaifu akiwa amebeba nafaka kubwa kuliko (hata) yeye mwenyewe, akijitahidi kupanda kwenye kilele cha ukuta.
“Nilipotizama kwa makini na kuhesabu kwa usahihi, nilibaini kwamba nafaka ilianguka kutoka kwenye kucha zake mara 67 kabla ya mchwa yule hatimaye kufanikiwa kufika na nafaka ile kwenye kilele cha ukuta.
Kuona jitihada hizi za mchwa kulinitia nguvu kubwa ambayo kamwe sitaisahau.” Nilisema “Ewe Taimur! Kwa namna yoyote wewe sio dhaifu kuliko mchwa. Inuka na rudi kazini. Niliinuka nikakusanya nguvu zangu hadi hatimaye nikaja kupata ujasiri nilionao.”1
Rejea:
1. Namunah –e- Maarif, Juz,1 uk. 174;
1. Akhlaq –e- Ijtmaae uk, 41

Comments