CHUKUA TAHADHARI KATIKA USULUHISHI

CHUKUA TAHADHARI KATIKA USULUHISHI
Abdul Malik amesema: Ulizuka mzozo baina ya Imam Baqir (a.s) na baadhi ya watoto wa Imam Hasan (a.s).
Nilimwendea Imam na nikamuomba niingilie katika jambo hilo ili niwasuluhishe, lakini Imam (a.s) alishauri: “Usiseme neno katika mzozo huu kwani tatizo letu ni kama lile la mzee kutoka katika Bani Israel, aliyekuwa na mabinti wawili. Mmoja wao aliolewa na mkulima wakati mwingine aliolewa na mfanyakazi. Wakati fulani aliamua kuwatembelea. Kwanza alimtembelea binti yake aliyekuwa mke wa mkulima na alipofika katika nyumba yake, aliuliza juu ya afya yake, binti alisema: “Baba mpendwa, mume wangu amelima eneo kubwa la ardhi na kama mvua ingenyesha tungekuwa ni matajiri wakubwa katika Bani Israil yote.” Kisha alipokwenda kwenye nyumba ya binti mwingine, ambaye mume wake alikuwa ni mfanyakazi, aliuliza juu ya afya yake. Binti alisema “Baba mpendwa, mume wangu amefinyanga vyungu kwa kiasi kikubwa na kama Mwenyezi Mungu angezuia mvua mpaka vyungu vikauke, tungekuwa matajiri kuliko Bani Israil wote.” Alipoondoka kutoka kwenye nyumba ya binti yake wa pili, aliomba: “Ewe Mungu! Fanya kama unavyoona inafaa, kwani katika hali hii, siwezi kumuombea yeyote kati yao.”
Kisha Imam akamniambia, “Wewe pia huwezi kuingilia katika jambo hili. Kuwa mwanagalifu, usije ukaonyesha utovu wa nidhamu katika upande mmojawapo. Jukumu lako kwetu, kwa sababu ya uhusiano wetu na Mtukufu Mtume, ni kututendea tofauti na kwa heshima.”
Rejea:
1. Daastan-ha Wa Panda-ha Juzu ya 1 ukurasa wa 134,
2. Raudhah al-Kafi, uk. 85.

Comments