KUSULUHISHA PANDE ZINAZOZOZANA
Mwenyezi Mungu Mwenye hekma, amesema: “Na ikiwa pande mbili za waumini zitakuwa katika ugomvi, rejesheni amani baina ya pande mbili hizo.” (Suratul Hujurat; 49: 9)
Imam Sadiq (a.s) anasema:
“Kupatanisha baina ya watu wawili (wanaozozana) ni bora zaidi kwangu kuliko kutoa dinari mbili katika sadaka.”1
“Kupatanisha baina ya watu wawili (wanaozozana) ni bora zaidi kwangu kuliko kutoa dinari mbili katika sadaka.”1
Maelezo Mafupi:
Moja ya matendo ya wajibu yanayotuwajibikia ni kuzikagua na kuzirekebisha roho zetu. Mpaka mtu atakapojirekebisha yeye mwenyewe ndipo atakapoweza kuleta marekebisho kwa wengine. Kujaribu au kufanikiwa kuleta usuluhishi baina ya ndugu katika imani, ndugu, au majirani, ni jambo linalopendwa sana na Mwenyezi Mungu.
Moja ya matendo ya wajibu yanayotuwajibikia ni kuzikagua na kuzirekebisha roho zetu. Mpaka mtu atakapojirekebisha yeye mwenyewe ndipo atakapoweza kuleta marekebisho kwa wengine. Kujaribu au kufanikiwa kuleta usuluhishi baina ya ndugu katika imani, ndugu, au majirani, ni jambo linalopendwa sana na Mwenyezi Mungu.
Kwa lengo la kuimarisha umoja na maelewano badala ya utengano na mifarakano ni muhimu kufanya kila jitihada kuleta suluhu. Kwa kweli katika baadhi ya kesi, huruhusiwa (hata) kutumia uongo mweupe. Wakati mwingine hufikia hata kuwa wajibu ili chuki ife na faraka iishe.
Rejea: Al-kafi, juz. 2, uk. 167
Huo ni usuluhishi. Hiyo itakuwa na maana kuwa kinyume chake ni dhambi kubwa. Tabia za baadhi ya watu kuzua uongo dhidi ya watu wengine au tabia ya kuwachonganisha watu ili wagombane au wasikubalike katika jamii ni hatari na dhambi kubwa. Tujiepushe na watu wa namna hii.
Tusiseme isipokuwa yaliyo ya kweli tena kwa nia ya kuwafundisha watu tu, endepo kama kuna sintofahamu au yanaweza kuleta mzozo ni bora tukae kimya hata kama ukisemacho ni ukweli.
Haikubaliki mbele za Allah Mtu fulani akijifanya ni mwislamu amtungie uongo mwislamu mwingine au atengeneza video, audio au picha ili kuipotosha imani ya mtu mwingine ili aonekane mbaya katika jamii. Waendao haya watalipwa vilivyo na Mola wetu.
Hapa nina kusudia baadhi ya watu wanaojiita waislamu, hutunga uongo na kuwasingizia mashia. Kiasi kwamba ukiwauliza hayo uyasemayo uliwahi kuyasikia mwenyewe, anasema hapana. Ukimuliza kwa nini usiyasikia na wakati unaishi na mashia, anajibu mashia hufanya taqiyyah. Huu ni ushetani. Mashia hawawezi kufanya taqiyyah kwako, wewe ni nani mpaka mashia wafanya taqiyyah mbele yako? Au hujui maana ya taqiyyah? Na kama hujui ni bora uulize badala ya kuzua uongo dhidi ya ndugu zako mashia.
Waislamu wote wa Afrika mashariki tunafanya taqiyyah. Kwa sababu Qur’an imetuagiza kuhukumu kwayo. Na asiyehukumu kwa Qur’an ni kafir. Je ninyi mnaoshutumu taqiyyah mmekwisha hukumu kwa Qur’an? Kama umeshindwa kufanya hivyo na bado unakwenda kwenye mahakama za kisekula, huoni kuwa hiyo ni taqiyyah. Kwa taarifa yako taqiyyah maana yake ni kuificha imani yako pale unapoona kuwa maisha yako yako hatarini endapo kama utaidhihirisha.
Comments
Post a Comment