KWA NINI KUSOMA MAULIDI?
Waislamu husoma maulidi kwa
sababu mbalimbali. Kati ya hizo ni:
(i)
kuikumbuka na kuitukuza siku aliyozaliwa mbora wa
viumbe vyote, aliyetutoa vizani na kututia kwenye nuru;
(ii)
ni njia moja ya kutoa shukrani zetu kwa Allah kwa
neema hiyo;
(iii)
katika sherehe hizo, hupatikana fursa ya
kukumbushana maisha ya bwana mkubwa huyo na mafunzo yake;
(iv)
hupatikana fursa ya Waislamu wa madhihabi na mataifa
mbalimbali kushirikiana na kuziweka kando hitilafu zao;
(v)
Mikusanyiko hiyo huleta athari kwa wasio Waislamu ya
kuupenda Uislamu, na hata kusilimu.
(vi)
Mikusanyiko hiyo tuambatana na utoaji wa sadaka kwa
kutumia pesa na chakula. Hapo watu hupata thawabu zisizo na kifani.
(vii)
Pia mikusanyiko hii huambatana na kumsalia Mtume na
ninaamini kuwa kila mtu anajua kuwa Mtume (s.a.w.w) aliwahi kusema kuwa yeyote
atakaye mswalia mara moja yeye Mtume atamswalia mara kumi. Hii ni faida kubwa
kwa washerekeaji wa maulidi.
Comments
Post a Comment