MAULID HUAMBATANA NA KUMSIFU BWANA MTUME (S.A.W.W.):

MAULID HUAMBATANA NA KUMSIFU BWANA MTUME (S.A.W.W.):

Tunaposoma maisha yake, tunaambiwa kwamba, miongoni mwa maswahaba, walikuwako waliotunga mashairi ya kumsifu Bwana Mtume (s.a.w.w.) ambayo walikwenda nayo mbele zake na kumsomea.

Bwana Mtume (s.a.w.w.) hakuwafukuza watu hao wala hakuwakataza, bali aliwasikiliza na kuyafurahia yote waliyomsomea. Kwa kitendo hicho kwa hivyo, Bwana Mtume (s.a.w.w.) alitufungulia mlango wa kumsifu.

Tafauti ya pekee iliyoko baina ya maswahaba na sisi ni kwamba wao walimsifu machoni mwake, hali sisi tunamsifu akiwa hayuko na sisi kimwili. Sasa, kwa kitendo hiki, tunafanya jambo gani ambalo halikufanywa na maswahaba na kukubaliwa na mwenyewe Bwana Mtume (s.a.w.w.)?

Kama kufanya hivyo ni bid'a, basi sunna ni ipi?


Wewe kama unapenda kuwasifu mawahabi wenzio tu, basi tuachie sisi tumsifu Mtume wetu.

Comments