MAULID HUAMBATANA NA KUMSWALIA MTUME (S.A.W.W.):


 MAULID HUAMBATANA NA KUMSWALIA MTUME (S.A.W.W.):

Katika Qur'ani Tukufu (Sura 33:56), Mwenyezi Mungu anatuamrisha tumswalie Mtume Wake (s.a.w.w.) baada ya kutwambia kuwa Yeye na Malaika Wake hufanya hivyo pia.

Isitoshe! Na kila Ijumaa, khatibu hutukumbusha juu ya mimbari, kwa kututajia Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.), kuwa yoyote atakayemswalia yeye mara moja, Mwenyezi Mungu atamswalia (atamrehemu) mtu huyo mara kumi!

Jee, katika kikao kimoja tu cha maulidi, waliohudhuria humswalia Mtume (s.a.w.w.) mara ngapi? Zidisha mara hizo kwa kumi ujue Mwenyezi Mungu hukurehemu wewe mara ngapi katika kikao hicho.

Jee, ni lipi hapo -- kama halitakuwa sunna?


Tuendelee sana kusoma maulid, kila msikiti, kila nyumba, kila mitaa, kila kijiji, kila kata, kila tarafa, kila wilaya, kila mkoa na kila nchi. Ikiwezekana iwepo maulid ya kimataifa. Hii itatuongezea sana thawabu mbele za Allah, kumtangaza Mtume wetu na kufanya tabligh kwa wasiokuwa waislamu. 

Comments